Tuesday, September 8, 2015

DR SLAA AMEWASALITI WATANGANYIKA WANAO TAKA MABADILIKO AKIMBILIA MAREKANI KUJIFICHA UNAFIKI HAUFICHIKI,TAMAA YA FISI HUISHIA KULA MIFUPA


Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Dk. Willibrod Slaa amesema anakwenda Marekani pamoja na familia yake kwa mapumziko. Hata hivyo, taarifa zinasema Dk. Slaa amekwisha ondoka nchini Tanganyika kuelekea Marekani pamoja na familia yake tangu jana jioni. Huku akiwa Marekani kupumzika na kujiendeleza katika kozi fupi katika tasnia ya Sheria na Lugha, Dk. Slaa amesema nyumba yake itakuwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi.

Akizungumza katika mahojiano yaliyorushwa leo asubuhi na kituo cha televisheni cha Azam, mwanasiasa huyo amesema akiwa mapumzikoni Marekani, nyumba yake itakuwa inalindwa na Jeshi la Polisi kutokana na vitisho ambavyo amekumbana navyo tangu alipoamua kuachia ngazi Chadema.

“Ninatishiwa maisha, ni lazima nichukue tahadhari….., ninatishiwa kupigwa mawe. Ni kweli ninalindwa na usalama,” amesema Slaa akiwa anahojiwa na mwanahabari nguli, Tido Mhando.

Hata hivyo, Dk. Slaa ambaye ameshawahi kuwa mbunge wa Karatu mkoani Arusha amesema anashangazwa na taarifa zinazoenea kuwa amelala katika hoteli ya kifahari ya Serena jijini Dar es Salaam nchini hapa Tanganyika na kuhoji wakati wa uchaguzi mkuu, 2010, alilala mahali hapo lakini hakuna aliyehoji.

Kuhusu gharama alizotumia kufanya mkutano na wanahabari katika hoteli ya Serena, Dk. Slaa amesema, alipoenda Marekani katika ziara ya kichama, alizuru majimbo 13 na hakutumia fedha za Chadema bali marafiki zake ambao hakuwaweka bayana.

Dk. Slaa amesema licha ya kuwa ng’ambo katika kipindi hiki muhimu kwa taifa, ataendelea kufuatilia yanayojiri nchini. Ameahidi kurudi kupiga kura muda ukifika.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment