Friday, September 4, 2015

NCHINI TANGANYIKA MASWALI MAZITO YAMUELEMEA DR SLAA. DR SLAA PROF LIPUMBA JE SASA WAO NDIO WANATUMIWA KUIBOMOWA UKAWA....?? KWA NINI WAKISHAKUJING;ATUA HUKIMBIA NCHI...??


Nani alilipia mamilioni ya ukumbi hoteli......?? Nani alilipia matangazo ‘live’ katika televisheni....?? Kwa nini atake makada CCM wamsaidie....?? Kulikoni Mwakyembe kuonekana hotelini kabla...?? Iweje amkomalie Lowassa na kutomgusa Magufuli....?? Iweje maofisa serikali wamuandalie mkutano wake....?? Mkutano wake wagharimu milioni 80 yeye kazitowa wapi au ni nani aliye mpa...??
Siku moja tu baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, kutangaza kujing’atua katika siasa huku akiwashushia tuhuma nzito viongozi mbalimbali akiwamo waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa, maswali kadhaa yameibuka juu ya hatua ya kiongozi huyo na kama ni mkweli na msafi basi ayajibu.
Uchunguzi uliofanywa na wandishi mbali mbali wa magazeti na habari na blog kwa ushirikiano mkumbwa ili kuwafikishi wananchi habari nzuri na kuwa juwa viongozi wenye sura mbili jana ulibaini kuwa mijadala mbalimbali imeibuka kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na hatua hiyo ya Dk. Slaa, huku baadhi ya viongozi aliokuwa nao katika kambi ya upinzani wakihoji maswali kadhaa yasiyo na majibu ya wazi kuhusiana na mkutano wake wa juzi kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam nchini Tanganyika. Mkutano wa Dk. Slaa unakadiriwa kugharimu takribani shilingi milioni 80 kulingana na takwimu zilivyokusanywa na wandishi mbali mbali hapo jana. Katika mkutano huo aliozungumza na waandishi wa habari kwa takriban masaa mawili, Slaa alitumia muda mwingi kumshambulia Lowassa aliyeteuliwa na Chadema kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika ((Tanzania)) Zanzibar akiwakilisha pia vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa). Mwenyekiti mwenza wa Ukawa unaoundwa na Chadema, Chama cha Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi na National League for Democracy(NLD), James Mbatia, ni miongoni mwa watu kadhaa walioibua maswali yasiyo na majibu ya wazi kuhusiana na mkutano wa Dk. Slaa. Akizungumzia Dk. Slaa kumhusisha Lowassa na kashfa ya Richmond, Mbatia alisema hizo ni njama za kutaka kuwaondoa katika harakati za kampeni za uchaguzi mkuu na kuhoji sababu za katibu huyo wa zamani wa Chadema kujitokeza juzi na kutoa tuhuma za kashfa hiyo ya mwaka 2008, huku akiacha baadhi ya kashfa kubwa za ufisadi zilizotikisa nchi.

Alitaja baadhi ya kashfa ambazo zilitikisa nchi kuwa ni pamoja na ile ya Tegeta Escrow ambayo kesi dhidi ya wahusika zilipelekwa kwenye vyombo vya sheria, Meremeta na ile ya wizi wa mabilioni ya shilingi toka benki kuu kupitia akaunti maalumu ya madeni ya nje (EPA). Mbatia alishangaa Dk. Slaa kutozizungumzia kabisa kashfa hizo kama kweli ana ajenda ya kupambana na ufisadi na kusisitiza kwamba kulikuwa na njama ya kuwatoa kwenye ajenda ya kampeni za uchaguzi. “Hawa wanataka kututoa kwenye reli ili tuanze kujibizana. Hatuna haja ya kumjadili,” alisema Mbatia Akieleza kuhusu kuwania urais kupitia Ukawa, alisema Dk. Slaa ambaye alipitishwa na Chadema kushindana na wenzake kutoka Cuf (Prof. Lipumba) na Dk. Kahangwa wa NCCR-Mageuzi, alikuwa akililia urais kwa kudai kuwa yeye ndiye bora kuliko wenzake na kufanya kikao kilichomalizika usiku Juni 17 mwaka huu kuvunjika, hivyo siyo sahihi kudai kwamba hakuwahi kuutaka urais. Kwa mujibu wa Mbatia, Lowassa baada ya kujiuzulu akiwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kama alithibitika kuwa na kesi ya kujibu, angeweza kushtakiwa kwani Waziri Mkuu anapokuwa nje ya nafasi hiyo, hana kinga ya kumzuia kushtakiwa. Alisema Waziri Mkuu kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika ((Tanzania)) Zanzibar ya mwaka 1977, Ibara ya 33, anatekeleza na kuwajibika kwa majukumu yanayotolewa na Rais.

Pia alipinga madai ya  Dk. Slaa kwamba Lowassa alisema angekuja na wenyeviti wa mikoa na wa wilaya wa CCM wakati wa kuhamia Chadema kuwa  si ya kweli. Alisema Dk. Slaa pamoja na wenyeviti wenza wa Ukawa akiwamo yeye mwenyewe (Mbatia) walishiriki  bega kwa bega katika mchakato wote wa kumleta Lowassa. Alisema Lowassa hakutoa kauli hiyo kwamba angekuja na viongozi hao wa CCM, bali alipokuwa bado katika chama hicho hao walikuwa ni miongoni mwa waliokuwa wanamuunga mkono. Mbatia alisema Dk. Slaa alikuwa akiulilia urais na kusema kuwa  yeye ndiye bora kuliko wenzake na kufanya kikao kilichomalizika usiku  Juni 17 mwaka huu kuvunjika. Alisema Dk. Slaa ndiye aliyesema asitangazwe kuwa mgombea kupitia Ukawa  Julai 14 mwaka huu mpaka baada ya siku saba ili kulifanya tukio hilo kuwa la kihistoria. Mbatia aliwataka wananchi kuepukana na hoja hizo ambazo ni nyepesi, kwani Ukawa wanasimamia uzalendo, utu, uadilifu, umoja na uwajibikaji. Kuhusu wito wa mdahalo kuzungumzia suala la Richmond, alisema wapo tayari lakini hawawezi kumruhusu mgombea wao Lowassa kushiriki kwani hiyo ni mbinu ya kuwataka watoke kwenye reli ya kuendelea na kampeni za uchaguzi mkuu. “Hawa wanataka kututoa kwenye reli ili tuanze kujibizana. Hatuna haja ya kumjadili,” alisema Mbatia. Aidha wachangiaji mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii nao waliibua maswali kadhaa kuhusiana na hatua hiyo ya Dk. Slaa. Wakati maswali kadhaa yakiibuka, jana kulikuwa na taarifa ambazo haikuweza kuzithibitisha moja kwa moja, kuhusu kutoweka kwa Dk. Slaa tena, ambaye inadaiwa aliondoka nchini jana tusisahau kuwa Prof Lip Lip LIpumba alifanya hivi hivi alitisha wandisha akajiuzulu akakimbia nchi akenda Rwanda kisha akarudi na huyu Slaa anafanya hayo hayo. Hata hivyo, Tulipojaribu kumtafuta Dk. Slaa kuhusiana na habari za kukimbilia nje, simu yake jana ilikuwa ikipokelewa na mwanamke ambaye alikana kwamba hiyo siyo namba ya Mwanasiasa huyo.

MASWALI YALIYOIBULIWA
Baadhi ya maswali yaliyoibua kizungumkuti kuhusiana na mkutano wa Dk. Slaa juzi ni pamoja na mlipaji wa gharama za ukumbi wenye hadhi ya juu wa hoteli ya Serena; mlipaji wa gharama za matangazo ya moja kwa moja kwenye televisheni tatu; kauli yake ya kutaka asaidiwe na makada wa CCM – Dk. Harrison Mwakyembe na Samuel Sitta katika kujenga hoja za kudhihirisha kuwa Lowassa alihusika na Richmond. Kadhalika, maswali mengine kuhusiana na mkutano wa juzi wa Slaa ni pamoja na swali kwamba je, ni kwa nini alimshambulia zaidi mgombea wa Ukawa, Lowassa na kisha kutomgusa hata kidogo mgombea wa CCM, John Magufuli...? Na kwamba je, ni iweje maandalizi ya mkutano wake yahusishe baadhi ya maafisa wa serikali waliokuwa wakitumia simu za ofisi ya umma kuwaalika waandishi wa habari....?

MBOWE AJIBU KIAINA
“Safari ya Chadema ni sawa na treni, inayoanzia Dar es Salaam kwenda Kigoma. Njiani watu wakageuka, na wakaendelea kugeuka katika vituo vingine vya njiani. Sisi tunaendelea,” alisema.
“Chadema siyo mali ya Mbowe wala kiongozi yeyote. Anayefikiri yeye ni mkubwa hana nafasi… Kamati Kuu (CC) iliamua, na Mkutano Mkuu uliamua vilevile kuwa Lowassa awe mgombea wa nafasi ya urais. Kama kuna watu wana mawazo tofauti watatukuta mbele ya safari,” alisema Mbowe wakati akizungumza kwenye mkutano wa kampeni mjini Sumbawanga jana.

KILA MZANZIBARI ATAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment