Tuesday, September 15, 2015

RAISI KIKWETE WA NCHI YA TANGANYIKA ASEMA MHUSIKA WA SAKATA LA RICHMOND NI YULE ANAETEMBEA NA TUNDU LISSU KILA SIKU KWENYE KAMPENI


Rais Jakaya Kikwete wa nchi ya Tanganyika amesema anashangazwa na Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu a.k.a. Ronaldo kumtaka amtaje mhusika wa Richmond wakati mwenye Richmond yupo na anatembea naye mikoani. Kikwete aliyasema hayo jana wakati akiwaaga wananchi wa Kigoma katika Uwanja wa Lake Tanganyika na kumtaka Lissu amtaje mwenye Richmond.
 
“Endapo Tundu Lissu atashindwa kumtaja mwenye Richmond, nitatoka hadharani na kumtaja mwenyewe,” alisema Kikwete.
 
Kabla ya mkutano huo, Rais Kikwete wa nchi ya Tanganyika alifungua jengo la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, (NSSF) ambalo limejengwa kwa Sh7 bilioni. Akifungua jengo hilo, aliwaomba wawekezaji na mifuko ya kijamii kuiga mfano wa NSSF kwa kuwekeza katika sekta ya majengo kwa kuwa yanapendezesha mji. Kadhalika, Rais Kikwete alizindua jengo la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) pamoja na nyumba 36 za bei nafuu zilizopo katika eneo la Mlole, Kigoma Mjini.
 
Suala la Richmond imekuwa moja ya ajenda za chama cha CCM katika kampeni za urais hasa baada ya Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa aliyejiuzulu wadhifa huo kwa kashfa hiyo baada ya kuhamia upinzani CCM imekuwa hapo ndio mahali pao katika kila mkutano.
 
Kila sehemu ambako mgombea urais wa CCM anakwenda, suala hilo limekuwa likiibuliwa, huku Lowassa akisema yeye hakuhusika, bali alijiuzulu kuiokoa Serikali isianguke kwa kuwa ulikuwa uamuzi wa wakubwa.
 
Mgombea urais wa CCM, Pombe Magufuli amekuwa akienda mbali zaidi akisema akichaguliwa ataanzisha mahakama maalumu ya kushughulikia mafisadi wanaosababisha umaskini nchini tulitaka tu kujuwa ataanza na hao wa ESCROW na EPA au RICHMOND.....??

KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment