Saturday, October 31, 2015

NCHINI ZANZIBAR CHAMA CHA WANANCHI CUF KIMESIKITISHWA NA MATUKIO YA UTEGWAJI WA MABOMU


Naibu Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF nchini Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui akizungumza na vyombo vya habari kuhusiana na matukio ya miripuko ya mabomu.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Timu ya Ushindi ya chama cha wananchi CUF Mhe. Ismail Jussa Ladhu, akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Mhe. Nassor Ahmed Mazrui (kulia), kuzingumza na waandishi wa habari katika ofisi za Chama hicho Mtendeni nchini Zanzibar.

Chama Cha Wananchi CUF, kimeelezea kusikitishwa na matukio ya kuwatia hofu wananchi na kuhatarisha amani ya nchi. Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Chama hicho Mtendeni nchini Zanzibar, Naibu Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF hapa nchini Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui, ameyataja matukio hayo kuwa ni pamoja na miripuko inayoelezwa kuwa ni mabomu katika maeneo ya Mkunazini na Michenzani. Ameyataja matukio mengine kuwa ni uvamizi uliofanywa katika kisiwa cha Tumbatu ambao ulipelekea nyumba nne kutiwa moto na nyengine kadhaa kuvunjwa, sambamba na kupigwa na kujeruhiwa kwa wananchi 16 wa kisiwa hicho. Akifafanua kuhusu matukio ya miripuko, Mhe. Mazrui ameishauri Serikali kuwatafuta waliotega mabomu hayo kwa kutumia picha za kamera za ulinzi za CCTV ambazo zimesambazwa katika eneo lote la Mji Mkongwe.

Amesema bila ya kuchukuliwa kwa hatua wananchi wataendelea kuamini kuwa matukio hayo yamepangwa makusudi kwa lengo la kuwatia hofu wananchi washindwe kuendelea na shughuli zao za kimaisha.Wakati hayo yakiendelea, Mhe. Mazrui amesema juhudi kubwa zimeanza na zinaendelea vyema kwa kuzishirikisha jumuiya na taasisi za ndani na nje ya nchi, zikiwa na lengo la kukwamua mkwamo wa kisiasa unaoikumba Zanzibar hivi sasa. Nae Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Timu ya Ushindi CUF Mhe. Ismail Jussa Ladhu, amesema wanatiwa moyo na juhudi zinazoendelea, na kuwataka wananchi kuendelea kuwa wavumilivu na kudumisha amani.

KILA MZANZIBARI ATAKAE IPIGIA KURA CCM ILI IBAKI MADARAKANI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment