Friday, November 20, 2015

NCHINI MAREKANI WAZANZIBARI WAISHIYO NCHINI MAREKANI KESHO WATANDAMAANA CHINI YA UONGOZI WA ZADIA

zacadia

“Mbiu ya Mgambo Ikilia ina jambo”
Ndugu Wanachama wa ZADIA
Kufuatia maoni ya Wanachama ya kutaka tuitishe mkutano kujadili hali ya kisiasa huko nyumbani Zanzibar, Uongozi wa ZADIA ulikutana na kujadili swala hilo na kufikia maamuzi yafuatayo:
1- Tuandike barua ambayo itatumwa kwa Wajumbe wa Senenti na Baraza la Wawakili la Marekani. Na kila mwenye nafasi awasiliane na Mjumbe wa Seneti na Baraza la Wawakilishi katika eneo analoishi, kumtaka ashiriki kwa njia moja au nyengine kusaidia kukwamua mkwamo wa Kisiasa Zanzibar.
2-Tufanye maandamano Ikulu ya Marekani (White House) tukibeba mabango na Tamko rasmi la ZADIA kuhusu hali halisi ilivyo Zanzibar.
Kwa hivyo, Uongozi wa ZADIA unawaomba kuhudhuria kwenye maandamano hayo yatakayofanyika siku ya Jumamosi, tarehe 21/11/2015.
Tutaanza shughuli yetu saa sita mchana kwa majira ya Marekani ya Mashariki, mbele ya White House.
Maandamano haya pia yatawashirikisha wanamabadiliko wote kutoka nchini Tanzania na wapenda amani na Demokrasia kote ulimwenguni.
Wito unatolewa kujitokeza kwa wingi na kwa wakati. Tafadhali ukiipata taarifa hii mfikishie mwenzako.
Zanzibar kwanza.
Uongozi wa ZADIA.


KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment