Saturday, November 7, 2015

VIDEO-MOHAMMED ABOUD ASEMA LAZIMA LAZIMA UCHAGUZI URUDIWE-IKIWA ZANZIBAR NI MKEO BASI UTARUDIWA LAKINI KAMA ZANZIBAR NI NCHI HAURUDI NA OLE WAKO

Malumbano kuhusiana na Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar uliotangazwa kufutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, yamezidi kushika kasi baada ya Waziri katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kumshukia Maalim Seif huku akisisitiza kuwa ni lazima uchaguzi urudiwe.
Hata hivyo, mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (Cuf), Maalim Seif Shariff Hamad, amepinga kufutwa kwa uchaguzi huo aliodai alikuwa akielekea kushinda kwa asilimia 52.87 kutokana na karatasi za matokeo waliyopata kutoka katika vituo vyote vya kupigia kura huku CCM waliomsimamisha Dk. Ali Mohamed Shein, kutetea nafasi yake wakiunga mkono uamuzi wa Jecha. Jumla ya vyama nane vilivyoshiriki uchaguzi huo vinapinga kurudiwa kwake.
‘Wanaosema kuwa uchaguzi urejewe waachieni wenyewe. Sisi katika CUF hakuna msamiati huo kwa sasa. Kurejea uchaguzi huo siyo msimamo wetu,’ Maalim Seif alisema juzi kuwaambia wafuasi wa chama chake.
Kadhalika, waangalizi wa uchaguzi wa ndani na nje wametaka majumuisho ya kura ya uchaguzi huo uliosaidia kupatikana kwa matokeo ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yaliyomuwezesha Dk. John Magufuli wa CCM kushinda yaendelee kwani ulikuwa huru na wa haki na hakuna sababu za msingi kuufuta. Baadhi ya waangalizi hao ni wa kutoka Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya Ulaya (EU), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Jumuiya ya Madola na pia balozi za nchi kama Uingereza, Marekani na Ireland ya Kaskazini zimeisihi ZEC kuendelea na mchakato wa uchaguzi huo kwani hakukuwa na kasoro kubwa kiasi cha kuufuta.
Hata hivyo, Msemaji wa SMZ, ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud, amesema uchaguzi huo ni lazima lazima urudiwe kwani ‘haukuwa huru na wa haki’ kama alivyosema Jecha na pia kupongeza uamuzi huo aliodai umeihakikishia amani na utulivu Zanzibar hasa baada ya Maalim Seif kuibuka na kuonyesha kuwa ni yeye ndiye aliyeshinda. Waziri Aboud alisema kinachosubiriwa sasa ni ZEC kutangaza tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi huo na hivyo ni vyema vyama vyote vikatambua jambo hilo wakitaka wasitake. ‘Uchaguzi lazima lazima ufanyike Zanzibar, wananchi wapate haki yao kidemokrasia ya kuchagua viongozi wanaowataka baada ya uchaguzi wa mwanzo kuvurugika.îalisema Aboud.
‘Aliongeza kuwa alichofanya Jecha ni sahihi kwani alitumia busara na hekima kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu ili kulinda amani na Umoja wa Kitaifa na hadi sasa, uamuzi huo umesaidia kuivusha Zanzibar ikiwa katika hali ya amani baada ya uchaguzi.‘Mwenyekiti alitumia busara na hekima kufuta matokeo ya uchaguzi. Bila ya hivyo, Zanzibar ilikuwa katika hatari ya kumwagika damu,’ alisema Aboud na kuongeza:‘Kitendo cha mgombea wa CUF kujitangaza mshindi kabla ya matokeo ya tume kulisababisha hali ya kisiasa kuchafuka. Bila ya busara na hekima za mwenyekiti (Jecha) leo amani isingekuwapo Zanzibar,’ alisema Aboud.Aboud alisema licha ya Maalim Seif kujitangazia ushindi, pia uchaguzi wa Oktoba 25 ulitawaliwa na vitendo vya udanganyifu ikiwamo idadi ya wapigakura kuwa kubwa kuliko orodha ya wapigakura katika vituo.Kadhalika, alisema kitendo cha mgombea Maalim Seif kujitangaza mshindi kilichangia kuvuruga uchaguzi huo hasa baada ya maafisa wa ZEC kujikuta wakigawanyika na hivyo uamuzi wa kuufuta ulikuwa sahihi.
HAKUNA KAMPENI
Katika hatua nyingine, Aboud alisema uchaguzi huo utakaorudiwa baada ya ZEC kutangaza ratiba hautakuwa na kampeni kwa sababu kila chama kimefanya kampeni za kutosha; lakini wananchi watapewa elimu ya uraia ili kuhakikisha kuwa wanajitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa marejeo.Aidha, alisema watendaji wote wa ZEC au mamlaka yoyote, ambao watabainika kuhusika na kuvuruga uchaguzi wa Oktoba 25 watachukuliwa hatua za kisheria na uchunguzi mzito umeshaanza kufanyika kabla ya watu hao kukamatwa.Mkurugenzi wa ZEC, Salum Kassim Ali, alisema jana kuwa bado hawafahamu ratiba ya kufanyika kwa uchaguzi huo, lakini alisema wakati ukifika wananchi watajulishwa.
Vyama vinane kati ya 14 vilivyokuwa vimesimamisha wagombea vinapinga kurudiwa kwa uchaguzi huo, wakisema ulikuwa ‘huru na wa haki’ na kwamba, hakuna kifungu kinachompa Jecha mamlaka ya kufuta uchaguzi huo.Mbali na CUF, vyama vingine vinavyopinga kurudiwa uchaguzi ni DP, Chauma, NRA, Demokrasia Makini, Jahazi Asilia, SAU na ACT- Wazalendo.Aidha, vyama vingine mbali na CCM vinavyounga mkono kufutwa uchaguzi huo ni CCM, CCK, TLP na AFP. Chama cha Tadea ambacho pia kilishiriki uchaguzi huo bado hakijatoa msimamo wake.
TUME HAKI ZA BINADAMU, ACT
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Tom Nyaduga, amesema Jecha hakuwa na nguvu za kikatiba na kisheria za kufuta matokeo ya uchaguzi huo Oktoba 28 mwaka huu na hivyo haoni sababu ya kurudiwa kwa uchaguzi huo. Makamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Zanzibar, Ramadhani Suleiman Ramadhan, alitoa taarifa kwa vyombo vya habari jana akipinga pia kufutwa kwa uchaguzi huo.
Alisema hakuna sababu ya kuufuta uchaguzi huo kwa vile ulikuwa huru na wa haki katika hatua zake zote kwa mujibu wa viwango vya kitaifa na kimataifa kama ilivyothibitishwa na waangalizi wa uchaguzi wa ndani na nje.

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment