Sunday, December 20, 2015

CCM MAA MR NA MRS WENYE MARADHI YA BT WAKERWA NA NCHI YA MAREKANI KUZUI MABILLIONI


KABURINI KUNA KASHESHE NA KIYAMA KUNA NI BALAA Mhhha

Wakati Chama cha Mapinduzi kinapinga uamuzi wa Marekani wa kusitisha msaada kwa nchi ya Zanzibar na Tanganyika wa tilioni 1.5 kutokana na kufutwa kwa matokeo ya Uchauzio Mkuu wa  nchi ya Zanzibar lakini kura hizo hizo za wabunge na raisi wa Tanganyika wakazikubali na kumupisha Pombe Magufuli, Chama cha Wananchi CUF kimeunga mkono uamuzi huo na kutaka mshindi wa urais aliye shinda nchini Zanzibar atangazwe na kuapishwa ili kuondoa vikwazo vya kiuchumi. Msimamo huo ulitolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chama cha Wananchi (CUF),  Ismail Jussa Ladhu jana alipokuwa akizungumzia uamuzi wa Marekani kuzuia fedha za MCC hadi muafaka wa uchaguzi utakapopatiwa ufumbuzi pamoja na kuondoa sheria kandamizi ya makossa ya mitandao. Jussa alisema hakuna njia ya kunusuru Zanzibar ((Tanzania)) Tanganyika kuwekewa vikwazo vya kiuchumi ikiwemo kunyimwa misaada zaidi ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar kukubali kukamilisha uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka huu. Aidha alisema kuwa uamuzi wa Marekani wa kuzuia msaada unatoa fundisho kubwa kwa nchi nyigine kuheshimu mashariti ya kunufaika na fedha za MCC ikiwemo kulinda misingi ya Demokrasia na Utawala bora.
Jussa alisema matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa nchi ya Zanzibar yalifutwa kwa ubabe na Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya Zanzibar baada ya kuona CCM wapo katika hatari ya kuanguka lakini hakuna kifungu cha Katiba kinachompa uwezo huo. Alisema msimamo wa CUF utaendelea kubakia palepale pamoja na kufanyika kwa mazungumzo ya kutafuta muafaka wa uchaguzi, ZEC warudi kazini wakamilishe kuhakiki na kutangaza matokeo na mshindi wa uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka huu. Alisema kuwa kuna kikundi cha watu wachache nchini Zanzibar ndiyo hawataki kuona mabadiliko yakitokea ya kiutawala hapa nchini Zanzibar licha ya CCM kushindwa kufikia malengo ya Uchaguzi Mkuu mwaka huu.“Kuna kikundi cha watu Zanzibar hakitaki kuona mabadiliko ya kiutawala kwa maslahi yao binafsi licha ya CCM kuanguka katika uchaguzi wa Oktoba 25 Mwaka huu,”alisema Jussa. Alisema kuwa kadhia ya uchaguzi wa nchi ya Zanzibar imesababisha madhara makubwa ikiwemo wananchi kuishi katika mazingira ya wasiwasi pamoja na kupanda kwa gharama za maisha visiwani humo. Jussa alisema hakuna sababu kwa Viongozi wa CCM kuwa na wasiwasi wa kupoteza vyeo wakati marekebisho ya kumi ya Katiba ya nchi ya Zanzibar yameweka mfumo mzuri wa kuunda serikali ya pamoja na wao kunufaika kama CUF ilivyonufaka baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Aidha, alisema CUF haiko tayari kuona Uchaguzi Mkuu unarudiwa hapa nchini Zanzibar kwa malengo ya kuibeba CCM licha ya kuanguka katika uchaguzi wa awali Visiwani humo. Naibu Katibu Mkuu wa CCM nchini Zanzibar Vuai Ali Vuai, alisema kuwa haikuwa mwafaka kwa Marekani kuzuia msaada huo wakati Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ilikuwa na hoja za msingi za kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 Mwaka huu. Alisema kuwa uchaguzi wa Oktoba 25 Mwaka huu ulipoteza sifa za kuwa uchaguzi huru na wa haki baada ya kutawaliwa na vitendo vya udaganyifu kinyume na misingi ya demokrasia na utawala bora. Alisema hana wasiwasi na Marekani kuwa hawajapata taarifa na vielelezo vya kuharibika kwa uchaguzi wa Zanzibar na iwapo watapata taarifa hizo watakubaliana na uamuzi wa ZEC wa kufuta matokeo ya uchaguzi huo. Alisema  uchaguzi huo ulitawaliwa na vitendo vya udaganyifu ikiwemo idadi ya wapiga kura kuzidi watu waliosajiliwa katika daftari la wapiga kura wa kudumu pamoja na mawalaka wa vyama kupigwa na kufukuzwa katika vituo vya kazi. “Ufumbuzi wa migogoro sio kuzuia misaada kwa sababu unawaumiza hadi watu wasiokuwa na hatia, cha muhimu ni  kutafuta njia ya mufaka za kuondoa matatizo.”alisema Vuai ali vuai Mr BT.

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment