Wednesday, December 9, 2015

MIAKA 52 YA UHURU WA NCHI YA ZANZIBAR

DECEMBER 10 1963 SIKU YA SHEREHE ZA UHURU WA NCHI YA ZANZIBAR

Kama ilivyo desturi ya hustoria kesho tarehe 10 December tunatimiza miaka 52 ya Uhuru wa nchi yetu ya Zanzibar.Mwaka 1963 Zanzibar ilipata uhuru wake kutoka kwa Mwingereza (Uingereza) chini ya utawala wa Sayyid Jamshid bin Abdalla bin Khalifa ambapo serikali yake ilikuwa ukiongozwa na Waziri Mkuu Sheikh Mohamed Shamte Hamad.Historia haufutiki hivyo kila Mzanzibar anayofursa ya kuisoma na kujifunza umuhimu wa siku hii. Pia ikiwezekana kuikumbuka.Kabla ya Uhuru Zanzibar ilikuwa na kipindi cha mpito, ambacho iliundwa serikali ya umoja wa kitaifa.Katika kipindi kifupi cha udumu wa serikali hii uliweza kufanya kadhaa na muhimu kwa nchi yetu, kama vile kuwa mwanachama wa UN, mwanachana wa Commonwealth, na taasisi nyengine za kimaitaifa.

Licha ya kuweko njama maalum ya kuifuta au kupotosha historia hii Wazalendo wa Zanzibar wataendelea kwa nguvu zote kuikumbuka na kuadhimisha kila ifikapo December 10, iwe ndani au nje ya Zanzibar.

Hongera Uhuru wa nchi ya Zanzibar

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment