Thursday, December 17, 2015

SPIKA WA BUNGE LA NCHI YA TANGANYIKA YUKO NCHINI INDIA KWA MATIBABU YALE YALE VIONGOZI WAKIUMWA NJE YA NCHI RAI KUFENI

Spika wa Bunge la nchi ya Tanganyika, Job Ndugai tayari asha anza kufunguwa listi za kuwa mgonjwa na yupo India kwa matibabu cheza na thulma weee. Katibu wa Bunge la nchi ya Tanganyika, Dk Thomas Kashililah alisema jana kuwa Ndugai yuko nje ya nchi kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake bila ya kusema amekwenda nchi gani wala ugonjwa unaomsumbua.

“Ni kweli Spika yupo nje, lakini alikwenda kwa ajili ya kufanya uchunguzi tu, siyo kwamba anaumwa sana, hapana ila hii ni mara ya pili kwenda kufanya uchunguzi huo. Hata ukitaka kuzungumza naye mpigie simu mtazungumza naye maana hali yake inaendelea vizuri na yuko salama,” alisema Dk Kashilila.

Balozi wa wao wa nchi ya Tanganyika nchini India, John Kijazi alipopigiwa simu ili kujua kama kiongozi huyo yuko huko, alisema:


“Ni kweli yuko hapa India kwa matibabu na anaendelea vizuri. Unaweza kumpigia wewe mwenyewe uzungumze naye.” Alisema Kijazi bila kuweka wazi kwamba yuko hospitali gani na nini hasa kinachomsumbua.

Ndugai hajaonekana hadharani, kwa muda mrefu, hata katika shughuli muhimu za kitaifa ambazo zimekuwa zikifanywa na Rais John Magufuli, hivyo kuacha maswali mengi kutoka kwa wapenda kuhalalisha haramu.Shughuli mojawapo ambayo Spika huyo hakuhudhuria ni ile ya kuapishwa mawaziri wapya au hayo majipu mapya Jumamosi iliyopita Ikulu, jijini Dar es Salaam nchini Tanganyika. Naibu Spika, Dk Tulia Akson ndiye alihudhuria.

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment