Thursday, March 24, 2016

CCM WALIO PELEKWA PEMBA KUPIGA KURA WAICHOKOZA CUF NA KUANZA KUSHEREHEKEA WAPEWA KICHAPO POLISI WAWAPIGA CUF


Jeshi la Polisi jana walitumia mabomu ya machozi zaidi ya chama cha wananchi CUF baada ya CCM kuanza kuwachokoza wananchi wa Pemba ambao ni CUF ndipo CUF walipo anza kuwakanya wananchi hao kutoka mrima Tanganyika walio jazwa huko Pemba kwenda kumpigia kura Shein kuanza kusherehekea ushindi bandia wa Shein ambao kaupata kwa kuwekwa na nguvu za kijeshi la kutoka mrima huko kwa Wakoloni Weusi Tanganyika,mrima hao katika kijiji cha Mjini Wingwi Wilaya ya Micheweni, Pemba. Akizungumza na Muandishi wetu aliyekuweko huko Pemba, Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Micheweni, Rashid Khalid Salim, alisema vurugu hizo zimesababishwa na wanachama wa CCM kutoka katika kijiji cha Kwale wilayani humo. Alisema baada ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (Zec) kutangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa marudio, wanachama wa CCM katika kijiji cha Kwale, walianza kukusanyika na ngoma zao na kuanza safari ya kuingia katika kijiji cha Mjini Wingi, sehemu ambayo ni ngome ya wanachama wa CUF, huku wakisherehekea kwa kurusha ‘vijembe’ (maneno ya kejeli) na matusi. “Pamoja na kutakiwa kuacha matusi wakati wakisherehekea ushindi wa Shein, waliendelea na kusababisha wenzao kupandwa na ghadhabu kuwachemka na kuanza kupigana,” alisema Mwenyekiti huyo.
Alisema baada ya kutokea vurugu hizo, wanachama wa CCM kutoka kijiji cha Kwale, walilazimika kukimbilia Kituo cha Polisi Micheweni. Alisema askari walipofika eneo la tukio, walianza kupiga mabomu ya kutoa machozi na kuvunja milango ya nyumba za watu. Mwenyekiti huyo alisema nyumba 15 zilivunjwa milango wakati wakiwasaka watu waliokuwa wakihusishwa na atii na vurugu hizo ambazo zilianza kufanyika saa 10:00 jioni na kuendelea hadi usiku juzi. Aidha, alisema kwa mujibu wa mabaki ya milipuko, jumla ya mabomu 27 yanadaiwa kupigwa mbali na nyumba kuvunjwa milango na kusababisha watu zaidi ya 28 kuyakimbia makazi yao katika kijiji hicho.“Watu wanne wamekamatwa akiwamo mtoto mwenye umri wa miaka 13, lakini wananchi wengi wamekimbia makazi yao na kukimbilia katika kisiwa cha Kojani na Maziwang’ombe,” alisema Rashid.
Hata hivyo, alisema jambo la kushagaza polisi wameamua kuwakamata watu waliofanyiwa fujo badala ya kuwakamata waliokuwa chanzo cha vurugu hizo. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Hassan Nassir, alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo na kwamba watu watano wanashikiliwa atii kwa uchunguzi wa kuhusika na tukio hilo. Hata hivyo, alikanusha kuvunjwa milango 15 pamoja na kutumika mabomu 27 kurejesha hali ya utulivu baada ya wananchi kuanza kupigana. Waliokamatwa katika mkasa huo ni Kombo Khalfan Faki, Salim Hassan Khamis, Mjawiri Faki, Khatib Dawa Juma na Assaa Bakar Ali, wakazi wa kijiji hicho. Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa huo, Omar Khamis Othman, alisema hali katika kijiji hicho imerejea kuwa ya kawaida na kuwataka wananchi kuendelea na sherehe za kumpongeza Shein bila ya kuvunja sheria. Alisema wananchi waliokimbia makazi yao na kukimbilia katika kisiwa cha Kojani na Maziwang’ombe, watakuwa ndiyo waliohusika na vurugu na kwamba raia mwema hana sababu ya kukimbia askari.
KISHA NYINYI MUNAYAITA MAPINDUZI MATUKUFU HIVI KWELI NYINYI MUNAJUWA UTUKUFU NI NINI AU DUNIA IMEWAVA KISAWA SAWA MPAKA MNAKUFURU

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment