Friday, March 18, 2016

KIOO CHAKO NA MOYO WAKO VITAKUAMBIYA TAREHE 21 MACHI 2016 WEWE NI SHEIN TUUU.

 
Jumatatu ya tarehe 21 Machi 2016, Shein ataamka mapema kisha atasimama mbele ya kioo chake kujiangalia. Ile taswira kwenye kioo itamuambia: “Wewe ni Shein tuuuu!” Mwangwi wa sauti hiyo utatoka nje na kumchoma moyoni, naye kwa hasira atajibu: “Hapana. Mimi sio Shein tu. Mimi ni Rais Dk. Ali Mohamed Shein, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, niliyechaguliwa na asilimia 70 ya kura halali.” Akikiangalia tena kioo, ile taswira itamuambia tena: “Wewe  Ali ni Sahaba mkubwa sana na Mohammed ni Mtume wa Mwenyezi Mungu hawawezi kuwa Madhali na kuuwa watu ovyo na kutesa watu ovyo ili tu wabaki madarakani hawawezi kwa hiyo Wewe ni Shein tuuu!” Ataamua kukiadhibu kioo chake mwenyewe – pengine kwa kukivunjilia mbali, pengine kwa kuamuru kihamishiwe stoo milele.
Hivyo ndivyo hali itakavyokuwa kwake kwa siku zote zitakazounda miaka mitano inayoanza sasa. Kila siku, atapaswa kukabiliana na kivuli chake mwenyewe, ambacho kitakuwa kinamsuta kwa kumueleza yeye ni nani hasa, naye kila siku atataka kuthibitisha vile anavyojidhani ndivyo alivyo.Tafauti na Rais Ali Mohamed Shein wa 2010 hadi 2015 japo kuwa alishindwa uchaguzi lakini aliye shinda alimridhia kuwepo hapo alipo na wananchi pia walimridhia kwa shingo upande kwa kumsikiliza kiongozi wao adhimu kuwa tunaelekea kwenye mafanikio ambaye ni Maalim Seif Shariff Hamad, huyu Shein wa 2016 na kuendelea atakuwa na miaka migumu mno maishani mwake. Sababu ni kuwa nafsi yake inajuwa kuwa alipo sipo na aliyepo hapo si yeye. Hata katika kilele cha kujitoa fahamu anachojikuta kuwa nacho, bado kuna kitu ndani yake kinamrejesha kwenye ukweli wa mambo na ukweli huo unamuonesha taswira ya kwenye kioo – kuwa ni Shein tuuu.
Jamii yako inapokumbwa na matatizo yanayotokana na dhuluma ya mwenye nguvu dhidi ya mnyonge, ile dhana waliyonayo wajiitao wasomi ya “kutokuwa na upande” huwa ni alama ya ujinga wao, kwa sababu huwa wanamsaidia dhalimu kwenye vita vyake dhidi ya mnyonge. Kushirikiana moja kwa moja na dhalimu dhidi ya mnyonge huwa ni ukatili.Namzungumzia myonge wa nchi ya Zanzibar ambaye tayari alishakuwa taabani kwa kuwa serikali yake iliamua kutumia makundi ya uhalifu wa kisiasa yanayolindwa na vyombo vya dola, yampige, yamtese na yamuharibie mali zake na hata kuumuwa. Vyombo hivyo vya dola, ambavyo kimsingi vilikuwa na wajibu wa kumlinda, tayari vilishamueleza kuwa yeye hasa ndiye muhalifu na hivyo asitazamie ulinzi wowote. Ndio ujumbe uliomo kwenye kauli ya Mkurugenzi wa Upelelezi, Salum Msangi, anaposema “wanaodai kupigwa na mazombi ni wahalifu ambao wamekutana na wahalifu wenzao.”
Kinachotokea nchini Zanzibar hivi sasa kinatuhitaji kuchagua upande upi tunasimama, nami nimechaguwa upande alio mnyonge ambaye, licha ya kutokuwa na uwezo wowote wa kujitetea, Serikali ya Jamhuri ya Muungano Feki wa kulazimishana kwa Majeshi na Mitutu wa Mkoloni Mweusi Tanganyika imeamua kummiminia wanajeshi wa vyombo vya ulinzi na usalama kila kona ya mji wake. Hadithi za kupigwa kwa watu wazima – wanaume na wanawake, kuchomewa moto nyumba zao, ofisi za vyama na vituo vya afya, maeneo ya kukusanyika, na kukamatwa kwa hadi watoto wa miaka 14 zimekuwa za kawaida sasa.Yote yanahusishwa na hicho kinachoitwa uchaguzi wa marudio wa tarehe 20 Machi wa Bandia, ambao lengo lake pekee ni kumpatia Shein jina la urais wa nchi ya Zanzibar na uwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Mimi nimechaguwa upande na wala sitakaa nikasema ninajipumbaza kusaka mizania ya mambo kwenye hili, kwa sababu si jambo lenye mizania. Amri ya Amiri Jeshi Mkuu wa Serikali ya Wakoloni Weusi Tanganyika, Rais Pombe Magufuli, kuwashughulikia ati waleta fyokofyoko nchi Zanzibar haiwezi kutiwa kwenye mizania na kauli za viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) waliolalamikia kuwa wamekuwa wakiteswa, kuadhibiwa na kudhalilishwa na sasa wamechoka. Kuchoka kwao hakuwezi kuwekwa sawa na kuzidi kuumizwa kwa wananchi wa nchi ya Zanzibar.
Mimi nimechaguwa upande wa kumuambia Shein kwamba ikiwa gharama za yeye kuitwa rais ni hizi tunazozishuhudia sasa, basi kioo na moyo wake vitaendelea kumkumbusha kuwa yeye ni Shein tuuu. Ataendelea kupigiwa ving’ora. Ataendelea kufungwa nyuzi za viatu. Ataendelea kupigiwa saluti. Ataendelea kwenda na kurudi Ikulu ingia toka na kujipumbaza. Lakini yote hayo hayatakuwa na maana ya kumfanya kweli kiongozi anayezitawala nafsi za wale anaodhani kuwa wako chini ya utawala wake. Kwao wao, yeye atabakia kuwa ni Shein tuuu kama anavyoonekana na kioo chake na moyo wake kuwa ni Shein tuuu.Nimechaguwa upande wa mnyonge aliyepanga foleni siku ya tarehe 25 Oktoba 2015 kutoka Bungi Miembe Mingi hadi Msuka Mtongani na akapaza sauti yake ya nani awe nani kwenye nafasi za uongozi wa nchi yake kwa miaka mitano hii. Nilimuona. Nilimsikia. Na hadi sasa nikifunga macho usiku gizani, naweza kuuhisi uwepo wake ndani yangu. Alikuwa sahihi wakati ule na yuko sahihi leo hii.Niko upande wa mnyonge huyu pale anaposema kuwa kwake uchaguzi ulishafanyika na kumalizika Jumapili ile ya Oktoba 25 na hautambui mwengine kabla ya mwaka 2020. Ikiwa leo hii anaadhibiwa kwa msimamo wake huo, basi mimi niko pamoja naye. Inawezekana, kuwa kwa sote wawili – mimi na yeye – tu wanyonge, basi kuwa kwangu pamoja naye kusipunguze chochote kwenye maumivu anayoelemezewa na utawala ambao hautaki kusikia neno “HAPANA” kutoka kwake. Lakini angalau nakumpe moyo kuwa hayuko peke yake, na kamwe hatokuwa.
 KISHA NYINYI MUNAYAITA MAPINDUZI MATUKUFU HIVI KWELI NYINYI MUNAJUWA UTUKUFU NI NINI AU DUNIA IMEWAVA KISAWA SAWA MPAKA MNAKUFURU

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO

No comments:

Post a Comment