Thursday, March 31, 2016

MATAIFA 10 YA MAGHARIBI YAIONYESHA TANZANIA NINI MAANA YA HAPA KAZI TU


Mataifa 10 ya Magharibi yamesema hayataendelea na ufadhili wao kwa bajeti ya serikali ya Tanzania. ((Tanganyika))
Baadhi ya nchi hizo ni Sweden na Ireland. Nchi hizo zinaendelea na msimamo huo ikiwa ni siku chache baada ya shirika la utoaji misaada la serikali ya marekani (MCC) kuondoa msaada wake wa dola 472 za ufadhili wa miradi ya maendeleo kwa nchi ya Tanganyika ((Tanzania.)) Bodi ya MCC ilisema hatua yake ilitokana na mzozo kuhusu uchaguzi wa nchi ya Zanzibar na utekelezwaji wa Sheria ya Uhalifu wa Mtandao.
Mataifa yaliyositisha ufadhili wao kwa bajeti ya nchi ya Tanganyika ((Tanzania)) hata hivyo hayajaeleza sababu ya kufanya hivyo. Ubalozi wa Sweden umethibitisha kwamba taifa hilo limesitisha ufadhili wake kwa bajeti ya ya Tanganyika ((Tanzania,)) lakini ukasisitiza kwamba hatua hiyo haihusiani na yaliyojiri katika uchaguzi wa nchi ya Zanzibar.

No comments:

Post a Comment