Friday, March 25, 2016

NCHINI TANGANYIKA MFALME WA SAUDI ARABIA AMEMUAHIDI RAIS MAGUFULI WA NCHI YA TANGANYIKA USHIRIKIANO MKUBWA SANA


WATANGANYIKA WAJENGA NCHI YAO SISI VINGANGANIZI WA MADARAKA JAPO WATU HAWAKUTAKI NA HAWAJAKUPIGIA KURA BADO UNANGANGANIA NA KUENDELEZA UBAGUZI WA MUARABU NA MUAFRIKA HIZBU MACHOTARA MAZOMBIA KUENDELEA KUPGA WATU,KUNAJISI WATU,KUIBA MALI ZA WATU NDIO MAENDELEA YA ZANZIBAR HAYA YANAYO LETWA NA MAPINDUZI DAIMA.

Mfalme wa Saudi Arabia Mtukufu Salman Bin Abdulaziz Al Saud amemhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika Dkt. John Pombe Magufuli, kuwa nchi yake imeichagua Tanganyika kuwa nchi ya kipaumbele katika mpango wake wa kuimarisha zaidi mahusiano na Afrika uliolenga kuendeleza na kukuza biashara, uwekezaji na kushiriki katika miradi ya maendeleo.

Ujumbe wa Mtukufu Salman Bin Abdulaziz Al Saud umewasilishwa kwa Rais Magufuli jana tarehe 24 Machi, 2016 na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mheshimiwa Adel Al Jubeir Ikulu Jijini Dar es salaam nchini Tanganyika.

Katika Salamu hizo pamoja na kumpongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa kuiongoza Serikali ya awamu ya tano ya Tanganyika, Mfalme Salman Bin Abdulaziz Al Saud amesema Saudia Arabia imedhamiria kukuza zaidi mahusiano kati yake na nchi ya Tanganyika ili kuwaletea manufaa makubwa wananchi.
Kwa upande wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemshukuru Mfalme wa Saudi Arabia kwa kumtumia ujumbe na kumpongeza kwa kuchaguliwa kuiongoza Tanganyika na amemhakikishia kuwa Serikali yake itafurahi kuona Saudi Arabia inashirikiana na Tanzania kutekeleza miradi mikubwa ikiwemo ujenzi wa Reli ya Kati na barabara.
Maeneo mengine ambayo Rais Magufuli na Waziri Adel Al Jubeir wameyazungumzia ni ushiriakiano kati ya Tanzania na Saudia Arabia katika kuendeleza Elimu, Utalii, Bandari na miundombinu.
Pamoja na kufanya Mazungumzo hayo, Rais Magufuli pia ameshuhudia utiaji saini wa mkataba kuhusu ushirikiano kati ya nchi ya Tanganyika na Saudi Arabia katika nyanja za Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Ufundi, Vijana na Michezo, ambapo kwa upande wa nchi ya Tanganyika mkataba huo umesainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Augustine Mahiga, na kwa upande wa Saudi Arabia umesainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mheshimiwa Adel Al Jubeir.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
24 Machi, 2016

No comments:

Post a Comment