Tuesday, March 22, 2016

POLE DA SALMA POLE SANA DA SALMA,DA SALMA AELEZEA JINSI ALIVYO TEKWA

Salma_
FREE ZANZIBAR PEOPLE FROM MKOLONI MWEUSI TUNA LAANI VIKALI VITENDO VYA KINYAMA KAMA HIVI VINAVYO ENDELEA KUFANYWA NA WANAO ITWA ATII WATU WASIO JULIKANA WAKATI JESHI LA POLISI LINAJUWA KILA KITU NA CHAMA CHA MAPINDUZI NDIO KINAFURAHIA KABISA MAMBO KAMA HAYA YAKITOKEA TUNASEMA HIVYO KWA SABABU LIKITOKE LOLOTE POLISI HARAKA HUWASHIKA WAPINZANI NA KUWASWEAKA JELA ILA YAKIWAPATA WAPINZANIA AU WANDISHA WA HABARI BASI JESHI LA POLISI HUWA KIPOFU NA KUJIDAI UCHUNGUZI UNAENDELEA.

Mwandishi wa Mwananchi Communications Limited (MCL), Salma Said akiwa ameshikiliwa na mwandishi mwenzake, Kelvin Matandiko alipokuwa akiondoka katika Kituo cha Polisi cha Kati baada ya kuhojiwa, juzi usiku. Picha na Omar Fungo Dar es Salaam nchini Tanganyika. Mwandishi wa habari wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) na DW, Salma Said aliye tekwa na wanaume wawili baada ya kumkamata na kumuingiza kwenye gari lao kisha kuondoka naye na kumpeleka kusikojulikana. Salma aliyetekwa Ijumaa iliyopita na watu hao katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akitokea nchini Zanzibar kwa ajili ya kuchunguzwa afya yake kwenye moja ya hospitali za jijini hapa Dar es Salaam, alisimulia mkasa huo jana mbele ya waandishi wa habari huku akimwaga machozi.
Alisema alipoteremka uwanjani hapo, alimpigia simu dereva wake amfuate na wakati akimsubiri, ndipo wakatokea watu hao. Salma alisema watu hao walimfunga mtandio wake mweusi usoni ili asibaini mahali walikokuwa wakimpeleka na kumfungia chumbani Alisema ndani ya chumba hicho kulikuwa na vitambaa. “Waliponiingiza ndani ya chumba kile siku ya kwanza, wakanifungua tambala usoni kwa hivyo nikawaona nyuso zao, mmoja alikuwa na kovu shavuni, mrefu na mwingine mweupe kidogo, waliniweka kule ndani bila kupata chakula chochote,” alisema. Salma alisema alitakiwa kurudi nchini Zanzibar kwa ajili ya kuripoti marudio ya Uchaguzi Mkuu wa marudio uliofanyika juzi, lakini alishindwa baada ya watu hao kumteka na kumfungia kwenye chumba hicho. Alidai kuwa watu hao walimwambia watamuachia baada ya uchaguzi huo kufanyika na mgombea wa CCM kutangazwa kuwa mshindi.
Katika mkutano huo na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za Baraza la Habari nchini Tanganyika(MCT), Salma aliongozana na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini Tanganyika (TEF), Theophil Makunga, Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga na Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Bara (THRDC), Onesmo Ole Ngurumwa, ambao kwa pamoja walieleza kupinga ukatili huo huku wakiliomba Jeshi la Polisi kuwasaka wahalifu waliohusika.“Walinisababishia maumivu makali, walinipiga mabuti na makofi huku wakiniambia maneno ya vitisho kama ilivyokuwa kwa Dk Ulimboka na Kibanda,” alisema Salma.
Kabla ya watekaji hao kumrudisha katika eneo walilokuwa wamemteka, Salma alidai kuwa watu hao walimpiga kila walipoingia na kutoka nje ya chumba alichowekwa na kumsababishia apumue kwa tabu. Akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kupata ufafanuzi wa taarifa za uvumi wa kujiteka mwenyewe, Salma alijibu swali hilo huku akidondosha machozi: “Hakuna sababu ya kusema uongo, mimi ni Mwislamu na dini yangu inakemea kufanya hivyo.” Pia, alisema amefanya kazi kwa miaka zaidi ya 20 na matukio ya vitisho yalianza na alianza kuyapata muda mrefu kwa kupigiwa simu, kutumiwa meseji na kufuatwa nyumbani kwake. Salma ambaye alizungumza huku akionyesha ushahidi wa meseji za makundi ya mitandao yanayojadili kufurahishwa na kutekwa kwake, alisema kujiteka ni kauli zisizokuwa na uhusiano wowote na ukweli, kwani alijitambulisha kuwa mwandishi mtetezi wa haki za binadamu na siasa ambazo zinazokinzana na maslahi ya wachache. Wakati huo huo; Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya jiji la Dar es Salaam huko nchini Tanganyika, Simon Siro alisema ni mapema kuzungumzia tukio la kutekwa kwa Salma kwa madai kuwa bado wanaendelea kufanya uchunguzi.

KISHA NYINYI MUNAYAITA MAPINDUZI MATUKUFU HIVI KWELI NYINYI MUNAJUWA UTUKUFU NI NINI AU DUNIA IMEWAVA KISAWA SAWA MPAKA MNAKUFURU

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment