Thursday, March 24, 2016

VIDEO-HATA UFANYE NINI WEWE NI SHEIN TUU TUMEWAONA WALIO KUPIGIA WAMEJA KATIKA VITUO KUKUPIGIA KURA


Wanaposema wahafidhina tuko tayari kufa njaa....??
Jee wamewakusudia nani wakufa njaa.....?? Sidhani kuwa makeke haya na majikazo na majivuno haya ni kwa wao kufa njaa no wao wala familia zao hawatakufa njaa. Nadhani wamekusudia wananchi wakawaida ambao walikataa na wanaendelea kuikataa CCM na vitimbi vyake vya Kutawala kimabavu na kibaguzi kwa kutumia jeshi la Mkoloni Mweusi Tanganyika Wamrimaa. Hii kauli ni kama kuwakejea wananchi kua kwavile mumeikataa CCM kwahio kufeni na njaa na sisi tutaindelea kuwanyonya ili tupate kuishi kwa hicho hicho tutakacho wakamua kutuka kwenu kama vili kodi na ushuru na kadhalika. Hakuna shaka kua Shein atakuwa na wakati mgumu katika utawala wake wakulazimisha ,kwani itakuwa ni utawala wakimabavu nguvu, kibaguzi kutokana na itikadi za kivyama na utakao shindwa kuheshimu sheria na haki za kibimadamu. Yote hayo yameshaanza kujitokeza siku tatu tu tulizoelekea kwenye uchaguzi tumeshuhudia vitimbi vingi na kabla hata ya uchaguzi pia tumeona vitimbi vingi sana. Uvamizi wa kijeshi watu kuteswa kubaguliwa kulazimishwa kupiga kura kwa vitisho na utekaji nyara na kuwaingilia kinguvu wananchi.
Serekali ukiona inatumia hali hio kwa raia wake  Basi ujuwe imepoteza STATUS yakua Serekali .Inabakia kuwa gange la kihuni kuwaonea raia wasio na hatia na wasio weza kujitetea. Kwa hali hio ndivyo itakavyokua Serekali ya Shein na Gainge lake la wahuni. Serekali ya Shein itakuwa ya mkono wa chuma kwavile imepoteza imani kwa wananchi na hivi sasa haina budi kulazimisha mambo.kinguvu nguvu na kukanya haki za binadamu. Tusahau kua tulipata unafuu wa serekali ya umoja wa kitaifa SUK au GNU hii total imeshakufa na imeuliwa maksudi na wahafidhina ili kukizi kiu yao na Mkoloni Mweusi Tanganyika hakuipenda SUK au GNU ndio maana yuko mkono kwa mkono kuiyuwa SUK au GNU. Sasa Serekali itakayokuweko kwa mujibu wa uchaguzi au uchafuzi wa Jecha Firauni Jecha ni Serekali ya chama kimoja na itikadi moja .Kwa hio watakao ingizwa na kuchaguliwa humo ni kada mawaziri wa CCM na mawakala wao wote ni gange la wahuni tu. Na katika uwajiri wa kazi utakuwa ni wa upendeleo kivyama na hilo limesha jitokeza katika upigaji kura wa juzi wajiriwa wa serekali walifosiwa kwa vitisho kufika hadi kuambiwa ama kazi au wapotelee mbali. Hawa kuwa na uhuru wao wa kuchagua mamuzi wanayo yataka ,wengine waliambiwa eti wende tu kwenye vituo ili kioo cha dunia kione watu wamejitokeza lakini kilichoko nyuma ya pazia ni chengine.
Nadhani ulimwengu umeshuhudia mara hii kilichoko nyuma ya pazia maana Maaalim Seif Sharrif Hamad aliwafunulia kuona. Ulimwengu ulichazoweleshwa kua Zanzibar imejigawa makundi mawili kutokana na historia yake ya nyuma ya vyama. Ulimwengu ulizowea kudanganywa kua matatizo ya Zanzibar ni U-Arabu na U-Afrika wakulinda mapinduzi. Hii ilikua ndio kasumba kubwa walio kua wakiisimamia na kua ngao yao wahafidhina ambao hawakubaliki kwa wananchi walio wengi wa nchi ya Zanzibar wenye kutaka mabadiliko na kupuza kasumba hizo zilizopitwa na wakati. Kwa hio ulimwengu umewashtukizia na umeshtukizia Mkoloni Mweusi Tanganyika ((Tanzania)) kwa kipindi cha nusu karne imekua ikitumia kivuli hicho ili kufunika maovu yao. Ndio kusema kwa hali viongozi wa CCM hawako mbali sana na THE HAGUE hapa Zanzibar na hata hao wa mrima pia Mkoloni Mweusi Tanganyika hawako mbali tena kuitembelea THE HAGUE hivi sasa jinsi watakavyo iongoza nchi ya Zanzibar kimabavu na kumlazimisha Punda kunywa maji. Hee Mungu ibariki nchi ya Zanzibar na watu wake na uwalinde wale viongozi wetu wenye uzalendo na wanao simamia haki ya Wazanzibar kwa ujumla .
KISHA NYINYI MUNAYAITA MAPINDUZI MATUKUFU HIVI KWELI NYINYI MUNAJUWA UTUKUFU NI NINI AU DUNIA IMEWAVA KISAWA SAWA MPAKA MNAKUFURU

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.


No comments:

Post a Comment