Friday, April 8, 2016

VIDEO-NANI KAMUUWA MZEE KARUME NA KWA NINI TANGANYIKA AKATUAMULIA RAISI AWE MZEE JUMBE NA SIO KANALI SEIF BAKARI.

Nani alimuua Mzee Karume na kwa nini.....???
John Gideon Okello alizaliwa 1937, katika Wilaya ya Lango nchini, Uganda na alifariki mwaka 1971 kijijini kwao Lango Uganda alikokwenda kutupwa na Julius Nyerere na Abeid Karume. Kifo chake kimeacha majonzi kwa wanamapinduzi walio hadaliwa kutoka kwenye nchi zao na kuja nchini Zanzibar kuja kuwapinduwa wazanzibari katika nchi yao lakini baada ya mapinduzi hayo wamejikuta moja moja wakifa na kuliwa na kufukuzwa katika walio dhani wakifanya mapinduzi watakuwa viongozi wakubwa kumbe walikuwa tu wakitumiliwa kama majibwa ya usasi, kwani licha yakuwa rais wa kwanza wa Zanzabar na Baba halisi wa Taifa la Zanzibar kwa Mapinduzi ya Zanzibar lakini Waafro + Shiraz hawa wamemezeshwa uongo kuwa Karume ati ndie baba yao.
Okello kafa masikini hata msiba wake umehudhuriwa na ndugu tu bila heshima yoyote ya kiukombozi huu ndio mwisho wa kwenda nchi za watu na kuuwa watu bure kwa kutengemea utakuwa kiongozi mkubwa huu ndio mwisho wake unakufa hata majirani hawajuwi kama umekufa.
Capt Yusuf Hamud ndie aliyetekeleza mauaji hayo, lakini bado hoja inasimama kuwa,
Nani alimuua Karume....?? au tusema ni nani hasa aliye taka Mzee karume auwawe na kwa kosa ngani mpaka wakataka auwawe Mzee karume....??
Hapa kuna dhana nne.,
Wapo wanaosema ni chuki za askari mamluki wa Okello, hawa wanaungwa mkono na Julius Nyerere, Na wapo wanaosema ni Julius Nyerere na Muungano wake feki kutaka kulazimisha ili waitawale nchi ya Zanzibar, hawa wanaungwa mkono na mzee Aboud Jumbe Mwinyi aliyefungwa kizuizini pale Mjimwema Kigamboni. Pia wapo wanaosema ni visasa vya ndugu aliowau Mzee Karume kipindi cha mpito tangu anyang’anye madaraka kwa Okello. Hapo bado jibu la kitendawili hiki ni gumu, hasa ukitazama hoja za kila upande ni nzito na zinatetea kwa nguvu!!!! Na wapo wanaosema yalikuwa mapinduzi ya jeshi.
Hoja za Shivji ni nzito sana, hoja za Prof Othuman ni nzito pia, Hoja za Lissu ni nzito pia na hoja za Joseph Mihangwa ni nzito.
Joseph Mihangwa anasema wazi.
Kwa mujibu wa taarifa za Usalama wa Taifa nchini Zanzibar, mipango ya “kupindua” Serikali ya Karume ilianza kusukwa tangu 1967 – 1972 ndani ya nchi ya Zanzibar na Tanganyika , ambako nyumba ya Abdulrahman Babu ilikuwa kituo cha mikutano ya Wazanzibari ya kupanga Mapinduzi hayo. Kama hivi ndivyo, Karume alikuwa na sababu tosha kumtaka Nyerere kumrejesha Babu nchini Zanzibar “kuhojiwa”, Februari 1972 lakini mbona hakumrejesha kama alivyo warejesha wengine kina Hanga na Twala na wengine wengi au nyerere alikuwa na mpango mwengine na Babu...??
Mkutano wa mwisho ulifanyika Aprili 2, 1972, ambapo ilikubaliwa Mapinduzi yatekelezwe Aprili 7, 1972, yakihusisha makundi mawili: kundi la Wazanzibari walio kuwa wakishi nchini Tanganyika, wengi wao wakiwa wanajeshi, na kundi la Wazanzibari ndani ya Zanzibar, likihusisha raia na wanajeshi pia. Pamoja na uamuzi huo, kikao kilitoa majukumu mazito kwa baadhi ya washiriki, ikiwa ni pamoja na Hamoud na Ahmada kupewa jukumu la kuiba silaha kutoka kambi ya kijeshi, Bavuai. Ilikubaliwa kuwa, Babu na wafuasi wake kutoka nchi ya Tanganyika wasafiri kwa mtumbwi kurudi nchini Zanzibar Aprili 6 kuamkia alfajiri ya Aprili 7, na kufikia eneo lililopo kati ya mitambo mikuu ya mawasiliano [Cable and Wireless] na Klabu Starehe.- Baada ya hapo, Babu abakie amejificha kwenye nyumba ya Hamoud Hamoud, iliyotizamana na Klabu Starehe eneo la Shangani, kusubiri saa ya mapambano kuwadia je kwa nini Babu alikuwa kama vile ni kiongozi mkuu wa Mapinduzi au Babu ndio aliyekwisha chaguliwa apinduliwe Mzee karume kisha Babu ndio awe Raisi wa nchi ya Zanzibar maana ni msomi......??
Kwa mujibu wa taarifa, Babu aliondoka jijini Dar es Salaam nchini Tanganyika kwa mtumbwi uliofungwa redio mbili za mawasiliano haya hapa pia tujiulize radio mbili za mawasiliano akiwasliana na nani katika hizo radio mbili.....??, jioni ya Aprili 6, safari iliyoelezwa kuwa ya “kuvua samaki”; wakati madhumuni halisi yalikuwa ni kuwafikisha Babu na wafuasi wake Visiwani usiku wa Aprili 6, kwa maandalizi kamili ya kupindua Serikali ya Mzee karume. Jioni hiyo, Aprili 6, Uongozi wa Jeshi uligundua upotevu wa silaha nyingi Kambini Bavuai je waligunduwa vipi na ni akina nani hao walio gunduwa mbona mpaka leo hatuwajuwi majina na wao walikuwa upande upi katika jeshi.....?? - Na ingawa uongozi ulikuwa bado haujamhusisha mtu yeyote, lakini Hamoud, Hamada na askari wengine walianza kufuatiliwa kwa siri. Yaelekea kufikia hapo, Babu alijulishwa na kuonywa kwa njia ya redio akiwa baharini, juu ya kugunduliwa kwa mpango mzima wa Mapinduzi; akakatiza safari na kurejea haraka Dar es Salaam hima nchini Tanganyika.- Haijulikani kama wafuasi wake walikuwa wamekwishafika Zanzibar au la; au kama nao walijulishwa na kurejea Dar es Salaam nchini Tanganyika au laa.  Ni nani aliye mjulisha hizo habari na huyo aliye mjulisha alimjulisha akiwa nchini Tanganyika au akimjulisha akiwa nchini Zanzibar...?? pia kwa nini Babu alikubali moja kwa moja kuvunja safari na kurudi nchini Tanganyika bila ya kuzngumza na Hamoud na Hamada ambao ndio washirika wake....??
Lakini kuwapo nchini Zanzibar wanajeshi kama Kanali Mahfoudh- (Mkurugenzi wa Operesheni JWTZ, Dar es Salaam nchini Tanganyika) na Luteni Hashil Seif (Kikosi cha Wanamaji, Ukonga, Dar es Salaam nchini Tanganyika) saa ya kuuawa Karume, kunaonyesha baadhi yao tayari walikuwa Zanzibar kusubiri wenzao hawa walikuwa wakubwa katika jeshi huko nchini Tanganyika kwa vyovyote vile Nyerere atakuwa anajuwa kama wapo nchini Zanzibar. Saa 12.00 asubuhi, Aprili 7; Ali Khatibu Chwaya (raia) alikwenda kwa Ali Mshangama Issa (afisa wa tatu, meli M.V. Afrika, mkazi wa Zizi la Ng’ombe,nchini Zanzibar), kumweleza juu ya kutowasili kwa kundi la Dar es Salaam la Wazanzibari walio subiriwa kuja kufanya mapinduzi nchini Zanzibar. Baadaye asubuhi hiyo, Ali Mshangama, Chwaya, Miraji Mpatani -(karani wa shirika moja, nchini Zanzibar), Mohammed Abdullah Baramia (Mtunza Bohari, Idara ya Elimu), Ahmada na Hamoud, walikutana nyumbani kwa Hamoud na kuonyesha kukerwa na kusikitishwa kwa kutowasili kwa wapanga mapinduzi kutoka Dar es Salaam huko nchini Tanganyika, hasa wakijua pia kwamba, silaha zilizoibwa bado zilikuwa nyumbani kwa Hamoud hazijerudishwa katika kambi ya Bavuai, na hatari ya kuwezakugunduliwa.
Ilipofika saa 6.00 adhuhuri siku hiyo, Mshangama, Hashil Seif, Amar Saad Salim, maarufu kama Kuku (afisa usafirishaji, Idara ya Siha, nchini Zanzibar) na Chwaya, walikutana nyumbani kwa Amar Saad ambako Mshangama, Hashil Seif na Baramia walipendekeza mpango wa kupindua Serikali uhairishwe hadi watakapopata taarifa tofauti kutoka Dar es Salaam nchini Tanganyika. Kwa hiyo, saa 9.00 mchana siku hiyo, saa mbili tu kabla ya kuuawa kwa Mzee Karume, Baramia alikwenda nyumbani kwa Hamoud eneo la Shangani kuwasilisha pendekezo hilo.- Alimkuta Miraji Mpatani nje ya nyumba na kumweleza Baramia kwamba, pamoja na kundi la Dar es Salaam kutowasili, Ahmada na Hamoud walishikilia Mapinduzi yafanyike tu siku hiyo, kwa sababu Ahmada alikuwa anatafutwa na maafisa wa Jeshi hapa pia tunaweza kujiuliza hao maafisa wa jeshi la polisi ni akina nani na walikuwa wanamtafuta Ahmad kwa nini na ni nani aliye wamuru wao watafute Ahmad kwa kosa gani na wana ushahdi gani wa hilo kosa mpaka wakanza kumtafuta....?? Je, ni kwa sababu hii Luteni Hamoud, Kapteni Ahmada na Chwaya waliamua kufanya Mapinduzi, licha ya wenzaokutaka yaahirishwe....?? Kwa mujibu wa mkakati wa Mapinduzi uliofikiwa Aprili 2, 1972, Suleiman Mohamed Abdullah Sisi (mwanajeshi wa JWTZ, mkazi wa Ilala Flats, Dar es Salaam nchini Tanganyika) alipangwa kuongoza utekaji wa kambi ya Jeshi, Mtoni, ambapo Kapteni Ahmada, alitakiwa kuteka kambi ya Jeshi, Bavuai, Makao Makuu ya Jeshi na Chuo cha Jeshi cha mafunzo ya Redio, vyote hivi viko eneo la Migombani.
Kituo cha Polisi cha Malindi kingeshambuliwa na kutekwa na kikundi chenye silaha kikiongozwa na Luteni Hamoud ambacho kingeweza kuteka magari yenye Redio za mawasiliano. Askari Yusufu Ramadhan angeongoza kikundi cha maafisa wa Polisi walioingizwa kwenye mpango huo na kuteka Kituo cha Polisi cha Ziwani. Amour Dughesh (mwanajeshi;wa hapa nchini Zanzibar), yeye angeteka Ikulu na kumkamata Mzee Karume, kisha kumpeleka Kituo cha Redio kumlazimisha atangaze kupinduliwa kwa Serikali yake ya Kidekteta .- Baada ya hapo, Kituo hicho kingeachwa chini ya udhibiti wa Badawi, Mpatani na Mohamed Said Mtendeni (mwandishi wa habari, gazeti la China, mkazi wa Vuga, Unguja). Uwanja wa Ndege ungetekwa na kikosi cha wanajeshi na baada ya hapo kingeachwa chini ya udhibiti wa Ali Sultan Issa (meneja wa Shirika la Mafuta, Zanzibar). Mpango huo ulilenga pia kuteka Makao Makuu ya Umoja wa Vijana wa ASP, ambayo yalikuwa pia Makao Makuu ya Idara ya Usalama wa Taifa nchini Zanzibar, ikiongozwa na Kanali Seif Bakari na kuwekwa chini ya udhibiti wa Mohamed Abdullah Baramia, Kapteni Khamis Abdullah Ameir, wa Makao Makuu ya Jeshi la nchi ya Zanzibar; yeye alipangwa kuzuia mashambulizi kutoka nje kama Mapinduzi yangefanikiwa.
Mapinduzi au mauaji ya Kisiasa.....??
Mapinduzi ni kitendo cha kutaka kubadili sawia hali, serikali au mfumo fulani wa kijamii kwa matumizi ya nguvu, ikiwa ni pamoja na kuondoa mhimili wa mfumo huo. Mapinduzi yanaweza kuwa kwa njia ya jeshi kama jeshi limetumika au ya kiraia kama raia walitumika, kama yalivyokuwa Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964 ya genge la wahuni walio danganywa kuwa wao ni wafrika na nchi ya Zanzibar ni ya wafrika wakamuwa kuwauwa Wazanzibari ambao wao pia ni wafrika japo kwa kuna walio changanya na wahindi warabu wapishiani n.k lakini bado ni wafrika. Mauaji ya Karume hayawezi kuitwa mapinduzi ya kijeshi wala ya kiraia kwa sababu kifo chake hakikubadili mfumo wala muundo wa serikali.- Haya yanaweza kuitwa mauaji ya kisiasa yenye lengo la kuondoa chanzo au mhimili wa kero katika jamii bila kubadili serikali hapa pia tunaweza kujiuliza je ni yeye tu Mzee Karume ndio aliyekuwa kero na viongozi wengine walikuwa ni wazuri kwa nchi ndio maana akauliwa peke yake au nchi jirani zilikuwa na choyo kwa Mzee Karume kuweza kuongoza nchi ya Zanzibar na kuijenga vizuri kabisa wala hakutaka ushauri wa mtu wala kiongozi wa nchi ya jirani ndio maana wakamuwa kumuuwa ili wauyuwe nchi ya Zanzibar kimaendeleo....?? Maana amejenga nyumba za michezani,kilimani na mambo mengi kama viwanda n.k. je hii ni sabau ya kuliwa maana nchi za jirani zilikuwa bado zimezorota kimaendelea ndio wakamuwa wamuuwe Mzee Karume....?? Mwanazuoni mahiri Barani Afrika, Profesa Ali Mazrui, anatafsiri mauaji ya kisiasa (political assassination) kuwa ni kitendo cha siri cha kutoa uhai wa mtu mashuhuri kisiasa, kinachofanywa na wakala asiye wa serikali; kwa sababu za kisiasa au zisizofahamika. Naye Profesa William Gutteridge wa Chuo Kikuu cha Aston, anasema mauaji ya kisiasa kuwa ni kitendo cha kutoa uhai wa mtu mashuhuri katika jamii kwa sababu za kisiasa na kinajumuisha pia jaribio la mapinduzi lililoshindwa na watu wengi kuuawa katika kutekeleza kilichokusudiwa.
Kwa mantiki hii, mauaji ya Mzee Karume, kama yalivyokuwa mauaji ya Rais Anwar Sadat wa Misri, kwa kupigwa risasi wakati akiangalia gwaride la jeshi lake, yalikuwa na lengo la kuiondolea jamii kero bila umuhimu wa kubadili serikali.- Katika mauaji kama hayo, mlengwa huwa mmoja tu kama chanzo au mhimili wa kero.Mzee Karume aliuawa kwa sababu ya utawala wa kimabavu au choyo cha nchi jirani kwa kutaka Mzee karume auliwe ili waitawala nchi ya Zanzibar....??, ukatili na ukiukaji wa haki za binadamu kama tulivyoona hapo juu; wakati Sadat aliuawa kwa kuisaliti jamii ya Kimisri, kwa kusaini Mkataba wa suluhu kati ya Misri na Israeli uliojulikana kama Camp David ili kusitisha harakati za Waarabu dhidi ya Uzayuni wa Kiyahudi. Sababu nyingine ilikuwa ni kukumbatia sera za kiuchumi za Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), hatua iliyoathiri maisha ya Wamisri kiuchumi na matarajio ya kijamii ya Waislamu nchini humo na Jumuiya pana ya Kiarabu kwa ujumla. Malengo ya mauaji ya Mzee Karume yanajidhihirisha kwa vielelezo kwa yale yaliyofuatia chini ya utawala wa mrithi wake, Alhaji Aboud Jumbe Mwinyi, aliyechukua uongozi Aprili 11, 1972. Baraza la Mapinduzi lililoketi Aprili 10 -11, 1972, pamoja na kumthibitisha Jumbe kuanzia Aprili 7, 1972 kuwa Rais wa nchi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza hilo, pia lilipitisha azimio la kudumisha, kulinda, kutetea na kuendeleza fikra, malengo ya kimapinduzi na sera alizoacha Mzee Karume. Hata hivyo, Wazanzibari wengi narudia tena Wazanzibari wengi walitaka Kanali Seif Bakari amrithi Mzee Karume kwa kuwa alikuwa mtu wa karibu zaidi kwa Mzee Karume kuliko Jumbe pia Seif Bakari ni Mzanzibari halisi kuliko Mzee Jumbe aliyefahamika kuwa alitokea nchini Tanganyika kwa hiyo Wazanzibari wengi walitaka Kanali Seif Bakari, kwamba ndiye pekee miongoni mwa Wazanzibari ambaye angeweza kuendeleza fikra za mwasisi huyo wa Taifa la Zanzibar swali linakuja kwa nini hawakusikilizwa ikiwa Wazanzibari wenyewe wanamtaka Kanali Seif Bakari awe ndio rais wao kwa nini hawakusikilizwa na kuanzia hapa ndio tunaona kuwa Wazanzibari wamekuwa wakiekewa na kuchaguliwa viongozi japo kuwa hawawataki lakini hulazimishwa hao hao na sio viongozi wanao wataka wao au wanao wachaguwa wao hata iwe kwa kura huu ndio ulikuwa mwanza wa Mzanzibari kunyimwa haki yake ya kuchaguwa kiongozi  wanae mtaka. Nyerere aliingilia kati akiwa na hoja kwamba, kwa kuwa Rais Mzee Karume aliuawa na mwanajeshi, kumteua Bakari ambaye alikuwa mwanajeshi kumrithi kiongozi wa kiraia, kungetafsiriwa kuwa mapinduzi ya kijeshi yaliyoweka mwanajeshi madarakani.- Hoja ya Nyerere ikashinda kwa nini ishinde nyerere na Wazanzibari nani ni bora kwa Zanzibar yeye ni kama nani kuleta hoja hapa ndio inasibidisha wazi kuwa nyerere alikuwa na plani kamili ya kuimaliza nchi ya Zanzibar.
Kwa kuanzia, Jumbe alifuta Amri ya Mzee Karume ya kutoagiza chakula na bidhaa nyingine kutoka nje; akaruhusu akiba ya fedha za kigeni kutumika kuagiza chakula kumaliza tatizo la njaa na upungufu wa vitu, jambo lililokuwa mwiko wakati wa Mzee Karume.Vivyo hivyo, kwa mara ya kwanza, Serikali ya Zanzibar iliruhusu wanafunzi 17 kutoka nchini Zanzibar, kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nchini Tanganyika kumbe ni mpango kamili utakao kuja kuwauwa wazanzibari kieleimu miaka ya mbelel kama hivi leo tunajione wanavyo felishwa na kunyimwa nafasi za masomo kwa makusudi na kuahidi kupeleka wengi zaidi kwa miaka hiyo na miaka ya sasa ni kuwakata kwa wengi. Desemba 1972, ASP kilifanya Mkutano Mkuu wake wa kwanza tangu 1962 uliohudhuriwa na wajumbe zaidi ya 900 kutoka nchini, Mwalimu Nyerere na viongozi wengine wa TANU, pamoja na wageni wengine kutoka nchi 12 za Kiafrika, wakiwamo wawakilishi wa chama cha MPLA cha Angola. Katika hotuba yake ya ufunguzi, Jumbe alilaani tawala za kimabavu na ubabe, ukandamizaji na matumizi mabaya ya vyombo vya dola dhidi ya raia, alisema:- Viongozi lazima wawatumikie watu, na si watu wawatumikie viongozi je leo hii CCM inafanya nini....?? Kwa maneno hayo, alikuwa amefungua milango ya demokrasia nchini Zanzibar kabla nchi zengine za bara la Afrika na hata nchi za jirani za karibu na nchi ya Zanzibar, utawala bora, uwajibikaji na kuongoza kwa mifano, tofauti na enzi za Mzee Karume. Februari 5, 1977, Nyerere na Mzee Jumbe waliunganisha vyama vyao, TANU na ASP je jumbe aliwauliza Wazanzibari je aliwachia wazanzibari wapige kura kukiuwa chama chao cha ASP na kumezwa na CCM au alijiamulia kama yeye ndio baba mwenye nyumba hii ni nchi sio nyumba yako utafanya utakavyo nchi sio hivyo, kuunda Chama cha Mapinduzi CCM, jambo ambalo lisingewezekana wakati wa Mzee Karume ambaye hata Muungano wenyewe aliweza kuusigina kwa kisigino cha nguvu hapa pia inatuonyesha kuwa Mzee jumbe aliekwa na Nyerere labda yeye alikuwa na moyo safi kwa wazanzibari lakini nyerere alikuwa katika mpango wake wakuimaliza nchi ya Zanzibar ndio maana alimkata Kanali Sief Bakari akamtaka Mzee Jumbe maana alijuwa Mzee Jumbe atamtumilia atakavyo akisha atamtema na naam hivyo ndivyo alivyo fanya alimtumilia Mzee Jumbe alipo maliza tu alipopataka akavuwa nguo zote na kumtupa mji mwema kigamboni anadhali Kanali Seif Bakari angelikubali upumbavu huu...??
Vivyo hivyo, mwaka 1979, Zanzibar ilijipatia Katiba yake ya kwanza baada ya Katiba ya Uhuru ya 1963, chini ya Serikali ya Mseto wa Zanzibar Nationalist Party (ZNP) na Zanzibar and Pemba Peoples Party (ZPPP).Ni wakati wa utawala wa Mzee Jumbe, Zanzibar ilipata Bunge (Baraza la Uwakilishi) lake la kwanza kwa njia ya uchaguzi, wakati kabla ya hapo, Mzee Karume aliapa pasingekuwa na uchaguzi nchini Zanzibar kwa miaka 50, kuanzia 1964 hadi 2014.Chini ya MzeeJumbe, kwa mara ya kwanza tangu 1964, wanasheria waliruhusiwa kufanya kazi nchini Zanzibar; watu hawakugongewa tena milango usiku na kupotea katika mazingira ya kutatanisha. Na tazama, yote yalifanywa kuwa mapya, ambapo isingewezekana chini ya utawala wa Rais Mzee Karume leo hii yametufikisha kuwa ni Koloni la nchi ya Tanganyika hatuna nchi tena wala hatuna viongozi tena wala hatuna wakombozi tena wala hatuna maendeleo tena wala hatu jeshi tena wala hatuna polisi tena wala hatuna hospitali tena wala hatuna kuishi kwa amani ni wasi wasi tu wala hatuna umoja wala hatuna maskilizano tena wala hatuna mashirikiano tena wala hatuna kupendana na kuoneana huruma tena wala hatuna wa kumlilia sisi tupo tupo tu basi tunapelekwa pelekwa tu na nchi ya Tanganyika wanavyo taka wao ndio hivyo hivyo toka siku aliyo uliwa Mzee Karume na kumkata Kanali Seif Bakari kuwa Raisi wa nchi ya Zanzibar hapo ndipo Wazanzibari walipo malizwa mpaka leo hii.
Nani alimuua Mzee Karume na kwa nini.......??

No comments:

Post a Comment