Friday, May 27, 2016

POLICCM NCHINI ZANZIBAR WAUNYAUNYA KUMHOJI RAIS, KIPENZI,LULU YA WAZANZIBAR MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD

UNGUJA NGANGARIPEMBA NGANGARI
Maalim Seif Sharif Hamad akiwa pamoja na Maofisa Wakuu wa PoliCCM, Zanzibar. Picha ni ya zamani tangu Maalim Seif akiwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Kama poliCCM nyinyi ni kweli Anzeni Kisonge,Borafya,Vuai ali Vuai,Shaka N.K.
TAARIFA kutoka Zanzibar, zinasema kwamba PoliCCM, wamefuta mahojiano na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad yaliyopangwa kufanyika Ijumaa, Mei 27, 2016 Ofisi Kuu za Polisi Ziwani, Unguja. Hakuna taarifa rasmi zilizotolewa za kufutwa kwa wito huo lakini, PolisiCCM imesema mahojiano yao na Maalim Seif, yatapangwa siku nyingine. Hata hivyo, baadhi ya watu wamesema kwamba, PoliCCM Zanzibar, wameakhirisha kumhoji Maalim Seif kutokana na kusoma alama za wakati: “PoliCCM Zanzibar, wamesoma alama za wakati wamegundua kwamba moto uliyotaka kuwaka Ijumaa, wasengeweza kuuzima na hali yengepelekea kuwa mwisho wa serikali ya mapinduzi na CCM yao chini ya uongozi wa Kibaraka Ali Mohamed Shein,” anasema kija mmoja kutoka mdodo-pilau, Kaskazini Unguja. “Umati tulikuwa tushajipanga…tushanuia kike kwa kiume mkubwa kwa mdogo kutoka kila pembe ya Unguja na kila anayeipenda Zanzibar,” anasema kijana wa mdodo-pilau, Kaskazini Unguja na kuhoji: “Kwa nini waliweza Tahrir Square, Egypt sisi tushindwe kupambana na vibaraka hawa?.” Maalim Seif, alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, kuanzia Novemba 2010 hadi Machi 20, 2016 baada ya uchaguzi haramu wa marudio kwa kuratibiwa na CCM na kuuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kama ilivyokuwa ikipendekezwa kwa muda mrefu na makada wa CCM. 
Aidha, watu wengi wamekuwa wakitoa maoni yao juu ya hatua hiyo ya poliCCM ya kumwita Maalim Seif kutaka kumuhoji kwamba ni hatua ya kisiasa zaidi kuliko majukumu na kazi za polisi za usalama wa raia na mali zao. Watu wanahoji: “Kwa nini Maskani ya Kisonge wamekuwa wakiandika juu ya ubao, kauli tata na chonganishi, kauli za ubaguzi na fitina dhidi ya wananchi wa Zanzibar, hakuna hata kiongozi mmoja wa maskani hiyo, aliyeitwa poliCCM kwa mahojiano. Baadhi ya wanasiasa kama, Borafya Mtumwa Silama, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini, Unguja amekuwa akitoa kauli za ubaguzi na matusi dhidi ya Maalim Seif, kuwatukana wapemba na waarabu, hajawahi kuitwa poliCCM kwa mahojiano. Hiyo ndiyo sababu inayowafanya baadhi ya watu kuhoji uweledi wa kazi za polisi wa Zanzibar. Huku hayo yakiendelea, imeelezwa baadhi ya maeneo Unguja na Pemba, wananchi wameanza visomo (dua) kumshitakia Mwenyezi Mungu juu ya madhila wanayopewa na Jeshi la PoliCCM kwa maelekezo kutoka kwa viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ na CCM). Wakati huo huo, wanasheria wa CUF wakishirikiana na wananchi katika sehemu mbalimbali Unguja na Pemba, wanaendelea na kazi ya kukusanya vielelezo na ushahidi juu ya vitendo vya ukatili dhidi ya binaadamu, kujipanga kwa mashitaka yaliyowasilishwa kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu, mjini The Hague.
KISHA NYINYI MUNAYAITA MAPINDUZI MATUKUFU HIVI KWELI NYINYI MUNAJUWA UTUKUFU NI NINI AU DUNIA IMEWAVA KISAWA SAWA MPAKA MNAKUFURU MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA KATUPINDUWA TENA WAZANZIBARI NA KUWEKA VIONGOZI WAWATAKAO WAO WAKINA BT TUNAENDELEA TENA KUKA CHINI YA SERIKALI YA KIKOLONI YA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA MPAKA MIAKA MITANO IMALIZIKE KISHA TUTIWE TENA KATIKA SHENGESHA LA UCHAGUZI NA KUPIGA KURA KISHA WAZANZIBARI WAPIGE KURA NA KUCHAGUWA VIONGOZI WAWATAKAO MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA ATAKUJA NA STYLE MPYA YA KUZIPIGA KURA ZA WAZANZIBARI CHINI NA KUTUEKEA VIONGOZI WAWATAKAO KISHA TUTAKA TENA CHINI NA KUSUBIRI UCHAGUZI WA 2025 MAMBO YATAKUWA HIVYO HIVYO KISHA TUTAKA CHINA NA KUSUBIRI UCHAGU WA WA 2030 TUKIWA HAI KAMA HATUKO TENA WATAKAO BAKI WATAFANYIWA TENA HIVYO HIVYO NA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA KISHA WATAKA CHINI WASUBIRI......>>> MPAKA KIYAMA KISIMAME BASI NI BORA TU TUKUBALI KUWA NDIO TUMEKUBALI KUWA CHINI YA MKONI MWEUSI TANGANYIKA KULIKO UPUMBAVU HUU WA UCHAGUZI AMBAO KILA MOJA WETU HAPA ZANZIBAR KAMA UCHAGUZI WA MARA HII HAUJAWASOMESHA WALA HATUTA SOMA TENA MILELE. 

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment