Wednesday, June 1, 2016

CCM IMAJI NYAKANYAKA NCHINI ZANZIBAR SASA ZAMU YA DOLA KUJARIBU KUMDHIBITA MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) visiwani Zanzibar kimeshindwa kumdhibiti Maalim Seif Sharif Hamad na sasa dola kutumika,
Wabunge Feki na Waharamu wa CCM kupitia Baraza la Wawakilishi Feki (BLW) visiwani humo jana walipitisha ati hoja kuwa Maalim Seif adhibitiwe na vyombo vya dola kwa madai ya kusababisha uchochezi kwa wananchi.
Hoja hiyo binafsi iliwasilishwa na Mtumwa Pea Yusuf, Mbunge wa Jimbo la Mpendae, Unguja akiitaka Serikali ya CCM na vyombo vyake vya dola ‘kumshughulikia’ Maalim Seif ambaye alikuwa mgombea urais visiwani humo kupitia Chama cha Wananchi (CUF) katika uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba mwaka jana.
Katika baraza hilo la upande mmoja (CCM), wajumbe wote walipitisha hoja hiyo kwa shangwe wakilenga kupunguza kasi ya Maalim Seif ambayo inamwathiri Shein katika serikali yake feki.
Tangu kumalizikwa kwa uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka jana na matokeo yake kuvurugwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kwa maslahi ya Shein ambaye ni mgombea wa CCM, Maalim Seif amekuwa mwiba visiwani humo na kuwanyima usingizi CCM na genge lao la Wahuni walio baka Demokrasi na sasa wengine wanabaka watoto wao kwa laaana zinavyo wandama.

No comments:

Post a Comment