Thursday, June 2, 2016

NCHINI ZANZIBAR MASHEIKH PEMBA WAVUNJA UKIMYA NA KUMPA KWELI ATI MUFTI ((ASTAHAFIRUH ALLAH HASTAHIKI KUITWA MUFTI WAKATI ANATUMILIWA NA CCM ))


MUFTI HII NI KWA AJILI YAKO IKIWA HUJAWAHI KUISIKIA ISIKILIZE KISHA WEWE UTAJUWA VYA KUFANYA 
Masheikh wa Pemba wavunja ukimya nchini Zanzibar.
Ujumbe wa ofisi ya Mufti wa nchi ya Zanzibar umefanya ziara 
na kukutana na baadhi ya Masheikh Kisiwani Pemba kwa 
lengo la kutaka kuzungumzia ati haki ya sasa inayoendelea 
kisiwani humo ambapo baadhi ya wananchi hususiana 
kuuziana  bidhaa na kukataa kuzikana kufuatia stafahamu 
iliyotokana na uchaguzi mkuu wa Octoba 25 ambapo 
inasemekana kilichofanyika ni dhulma ya wazi wa kupora 
ushindi wa Chama Cha CUF na kuwapa Chama cha CCM.

Ujumbe huo umefika Pemba na kuwataka Masheikh watumie 
taaluma yao ya dini kuwataka wananchi waondokane na hali 
ya kutengana na kuishi kama zamani. Haya soma kilichojiri 
katika kikao hicho ambacho Mufti wa Zanzibar Sheikh Saleh 
Omar Kaabi alikuwa miongoni mwao.
Katika maelezo yake Sheikh Saleh Kaabi na ujumbe wake 
aliokwenda nao wakiwataka Masheikh hao kuilimisha jamii 
kuishi vyema kwa upendo na mashirikiano kwa kutumia 
hadithi na aya za Quran Tukufu huku Masheikh wakielezwa 
kwamba wana umuhimu katika jamii.
Lakini Masheikh hao wamekuja juu na kusema kwamba 
hapawezekani kuwa na amani na upendo pasi na haki na 
uadilifu kutendeka. Mmoja wa masheikh ambao walipata 
nafasi ya kuchangia alisema na kuhoji kua tunawezaje 
kuyafikia mafanikio wakati hatujapita katika njia ya 
mafanikio...?? Huku akisistiza kuwa uislam hauangaliwi 
vipande vipande bali unapaswa kutizamwa kwa ukamilifu 
wake ambapo alisema kuwa hatuwezi kuangalia mwisho wa 
tatizo tu bali pia tunatakiwa kuangaia na chanzo cha tatizo.
Sheikh huyo alimkabili Sheikh Kaabi kwa kumpa fumbo la 
kiswahiki kwamba asitegemee kukoroga kinyesi halafu 
akategemea kusikia harufu mzuri puani mwake.
Sheikh mwengine naye alipata nafasi ya kuongea alisema 
kuwa Dk Shein kafanya dhulma kubwa na mikono yake 
inanuka damu na yeye mwenyewe anajua na kumtaka Mufti 
huyo wa Zanzibar Sheikh Saleh Kaabi amwambie Dk Shein 
arejeshe haki ya wananchi aliowadhulum ndipo amani na 
upendo utarudi visiwani humo.
Shekh Saleh pia alinasihiwa na kuambiwa kua aya na hadithi 
alizowatolea masheikh hao aende akawatolee na viongozi wa 
serikali kama vile Dk Shein, Balozi Seif na Maalim Seif Sharif 
Hamad huenda labda na wao kama binaadam wakafaham na 
wakaamua kutenda haki.
Huku Sheikh mmoja naye alihoji ni kwa nini mambo haya 
waambiwe wao wasiende kuambiwa hao waliosababisha 
matatizo haya ambao ni wenye mamlaka ya nchi na cyomvo 
vyake..? Alisema daima viongozi wa dini umuhimu wao siku 
zote hujulikana kipindi cha shida tu na matatizo lakini kukiwa 
hakuna vitu hivyo na nchi imetulia hawaitwi hata kupewa 
asante ingawa juhudi za kuituliza nchi kwa kiasi kikubwa 
hufanya na viongozi wa dini.
Katika suala la Mazombi na kamatakamata na utesaji pia 
baadhi ya Masheikh katika kikao hicho wamelizungumzia 
ambapo aliulizwa Sheikh Saleh Kaabi jee wananchi 
watafanyaje ikiwa mtu ambaye hana bunduki na uwezo 
wowote anateswa na kupigwa na kudhalilishwa na Jeshi la 
Polisi na Mazombi bila ya kosa..??Je ni haram kwao wao 
kuchukia tu wakati hatua za kuyakataa hayo zipo tatu kwa 
mujibu ya mafundisho ya Bwana Mtume...??
Pia aliulizwa tunawezaje kuwa na mapenzi ya kushirikiana na 
watu ambao waliwaweka mashekhe wetu ndani na kujisifia 
katika majukwaa ya kisiasa huku masheikhe hao na familia 
zao zikiendelea kupata tabu kwa mwaka wa tatu sasa...??
Hapo hapo mmoja wa Masheikhe hao akamwambia 
Sheikh Saleh kuwa kutokana na alivo anaamin kua kama 
angeamua kusimama usiku na kuwaombea dua tu 
masheikh wale basi Masheikh wale wangepata nusra ya 
Mwenyenzi Mungu lakini inaonekana hata hilo 
limeonekana limemshinda.
Aliendelea sheikh huyo kwa kusema kua watu waliomba dua 
nyingi ili kuinusuru Zanzibar na mambo mbali mbali lakini 
kuna viongozi wa kisiasa na serikali wakawa wanapita na 
kusema kua vi Alamtara vyenu havitowasaidia chochote 
(Astaghafurullah) sasa je mtu kama huyu ambaye anadharau 
na kuidhalilisha hadi Quran (maneno ya Allah) nae 
tushirikiane nae...??
Hakika Sheikh Saleh ambaye ni Mufti wa Zanzibar juzi 
alipata wakati mgumu sana ambapo hali kama hii aliwahi 
kukutana nayo wakati ule alipokwenda Pemba na kukutana 
na wanafunzi wake na kumueleza jukumu lake alilonalo 
serikalini ambapo Masheikh wa Jumuiya ya Uamsho 
wakiteseka Magerezani huku yeye akiwa amesalia 
madarakani.Masheikh hao wamesema hakuna nusura wala 
dua itakayoombwa ambayo itainusuru Zanzibar zaidi ya 
waliotenda dhambi hiyo ya dhulma ni kurejesha amana kwa 
waliowadhulumu ambao ni wananchi wa Unguja na Pemba.
Sheikh Saleh Kaabi aliinama chini mbele ya wanafunzi wake 
na kulia sana kwa uchungu baada ya kuelezwa atajibu nini 
mbele ya Allah hali ya kuwa Masheikh wanadhalilishwa 
Magerezani na kuthubutu kusimama mbele ya Mahakama na 
kuangusha vilio vya mateso na udhalilishaji wanaofanyiwa 
haki ya kuwa yeye bado yupo serikalini, hali hiyo ilimfanya 
achukue uamuzi wa kutaka kujiuzulu lakini wenye mamlaka 
walikataa uamuzi huo na hivyo bado anaendelea na wadhifa 
huo wa kuwa ndio kiongozi mkuu wa kidini serikalini.
Haizidi kwa mwenye kudhulumu ila khasara.
FREE ZANZIBAR PEOPLE FROM MKOLONI MWEUSI 
TUNASEMA HIVI:

 Mtume wetu alisema “MAN TASHABBAHA BIQAUMIN FAHUWA MINHU” 
mulikuwa mumuache tu ajiuzu kisha aende akatubiye huko 
maana toka mwaka jana yuko bega kwa bega na shein na 
haramu zote zifanywazu Unguja na Pemba na 
PoliCCM,MajeCCM,MazombiCCM na kuitishwa kura feki na 
uchaguzi feki kisha kujitagaza feki serikali feki yeye yumo na 
yuko pamoja nao leo ati anajidai kulia, Masheikh wako jela 
mwaka wa Tatu lini alisimama akasema mimi kama Kadhi 
Mkuu Nalani Vikali na kama Masheikh hawakupewa haki yao 
Najiuzulu lini kasema hivyo Mnafiki Mkubwa leo ajitia kulia 
nenda kamlilia Allah utubu na utake msamaha kwa Allah na 
ushukuru kakuziduwa kabla hujafa pia mwambie Shein 
ajiuzulu na arudishe haki ya watu ili Maalim apishwa kuwa 
ndio Rais aliye shinda Wazanzibari wanataka haki yao.

No comments:

Post a Comment