Monday, June 6, 2016

NCHINI ZANZIBAR VIKOSI VYA SMZ NA JESHI LA JKU WANATESA RAI NA KUWAPORA RAI PESA ZAO



HIZI PICHA NDIO DUBAI YA KWELI NA UTAKACHO SOMA HAPO CHINI MSOMAJI NDIO DUBAI YA SHEIN ALIYO WAAHADI WANANCHI NDIO DUBAI YAKE.
Baadhi ya askari wa vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), wakiwamo wa Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) wamedaiwa kuwatesa raia na kuwapora fedha wanapokuwa doria katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Mji wa Zanzibar.Hayo yalisemwa na Mwakilishi wa Jimbo la Chaani, Nadir Abdul¬latif Yussuf, wakati alipokuwa akichangia makadirio na matumizi ya Bajeti ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Vikosi vya SMZ) ya mwaka wa fedha 2016/2017.Alisema askari hao wameacha kufanya kazi yao ya kuimarisha doria na kuwahakikishia usalama raia na mali zao na badala yake wamekuwa wakikamata vyombo vya moto na kuwapekua mifukoni wahusika kabla ya kuwanyaganya fedha.“Mheshimiwa Spika, askari wa vikosi vya SMZ wamekuwa wakipiga watu, wanapekua mifukoni na kuchukua fedha. Hata mdogo wangu kafanyiwa kitendo kama hicho na kesi ipo katika kKtuo cha Polisi Madema,” alisema mwakilishi huyo huku ukumbi wa Baraza ukiwa kimya wakati akichangia.
Alisema kuwa vitendo hivyo vinafanywa na askari wachache na kuwaharibia wakubwa wao ambao wamekuwa wakitekeleza majukumu yao kwa uadilifu mkubwa visiwani humo.Alisema kuwa yeye binafsi alikamatwa na askari hao na kutakiwa kujieleza kwa nini amepita katika sehemu wasiyoruhusiwa kupita watu kwa miguu na kutishiwa kumwagiwa maji na pia kupewa adhabu ya kugalagala chini.Alisema baada ya kuwajengea hoja nzito, walishindwa kumpatia adhabu hiyo baada ya kufahamu wanazungumza na nani na kumwachia kuendelea na safari yake.“Mheshimiwa Spika, wafahamishwe nidham ya kazi, wasifanye kazi kwa kunyanyasa watu pamoja na kuwanyag’anya vitu,” alisema Mwakilishi huyo.Nadir alisema vitendo wanavyofanya baadhi ya askari hao vinakwenda kinyume cha misingi ya utawala wa sheria na kutaka serikali kukomesha vitendo vya askari kupora fedha wakijifanya wapo katika doria. Hata hivyo, Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Rashid Makame Shamsi alisema kuwa askari wa Vyuo vya mafunzo Zanzibar (Magereza) wanaishi katika mazingira magumu kutokana na nyumba wanazoishi kukabiriwa na uchakavu.
Aidha askari hao wanalazimika kuishi chumba kimoja familia yeye mke na watoto jambo halikubaliki katika misingi ya haki za binadamu chumba kimoja kuisha familia nzima na kusababisha haki ya faragha kupotea katika maisha ya kila siku.Katika hatua nyingine, Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu, Simai Mohamed Said, alisema kuwa wananchi wa Zanzibar wamekuwa wakipata shida wakati wa mvua kutokana na mji wa Zanzibar kukosekana kituo kikuu cha daladala pamoja na vituo vya gari za abiria na mabanda ya kujihifadhi kwa mvua na jua.Alisema kuwa gari katika manispaa ya mji wa Zanzibar zimekuwa zikisimama ovyo na kuhatarisha uslama wa wananchi na mali zao.Aliwambia Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW) kuwa hivi sasa, Zanzibar kuna tatizo kubwa la baadhi ya wanaume kukosa nidhamu kwa kukojoa ovyo na kusababisha uchafuzi wa mazingira.Alisema kutokana na kukosekana vyoo pamoja na kutunzwa vilivyokuwapo katika maeneo tofauti, Serikali imekuwa ikipoteza mapato mengi na kuna haja ya kufanyia kazi jambo hilo.

KISHA NYINYI MUNAYAITA MAPINDUZI MATUKUFU HIVI KWELI NYINYI MUNAJUWA UTUKUFU NI NINI AU DUNIA IMEWAVA KISAWA SAWA MPAKA MNAKUFURU MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA KATUPINDUWA TENA WAZANZIBARI NA KUWEKA VIONGOZI WAWATAKAO WAO WAKINA BT TUNAENDELEA TENA KUKA CHINI YA SERIKALI YA KIKOLONI YA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA MPAKA MIAKA MITANO IMALIZIKE KISHA TUTIWE TENA KATIKA SHENGESHA LA UCHAGUZI NA KUPIGA KURA KISHA WAZANZIBARI WAPIGE KURA NA KUCHAGUWA VIONGOZI WAWATAKAO MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA ATAKUJA NA STYLE MPYA YA KUZIPIGA KURA ZA WAZANZIBARI CHINI NA KUTUEKEA VIONGOZI WAWATAKAO KISHA TUTAKA TENA CHINI NA KUSUBIRI UCHAGUZI WA 2025 MAMBO YATAKUWA HIVYO HIVYO KISHA TUTAKA CHINA NA KUSUBIRI UCHAGU WA WA 2030 TUKIWA HAI KAMA HATUKO TENA WATAKAO BAKI WATAFANYIWA TENA HIVYO HIVYO NA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA KISHA WATAKA CHINI WASUBIRI......>>> MPAKA KIYAMA KISIMAME BASI NI BORA TU TUKUBALI KUWA NDIO TUMEKUBALI KUWA CHINI YA MKONI MWEUSI TANGANYIKA KULIKO UPUMBAVU HUU WA UCHAGUZI AMBAO KILA MOJA WETU HAPA ZANZIBAR KAMA UCHAGUZI WA MARA HII HAUJAWASOMESHA WALA HATUTA SOMA TENA MILELE. 

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment