Friday, June 10, 2016

RAMADHANI YOTE HII (SHEIN) UNASEMA MANENO KAMA HAYA


Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk.Ali Mohamed Shein amesema yeye siyo kiongozi dikteta kwani hajawani kumfukuza kiongozi yeyote wa kisiasa ndani ya chama chake kwa ajili ya kulinda maslahi binafsi.
Alimtaja Katibu Mkuu wa Chama cha CUF,Maalim Seif Sharif Hamad kuwa amekuwa akizua na kuzusha uongo kwa wafuasi wake kwa kuwaaminisha kwamba Dk.Shein ni kiongozi dikteta anayetawala Zanzibar kwa mabavu jambo ambalo sio la kweli.
Ufafanuzi huo wa Dk.Shein ameutoa wakati akizungumza na Mabalozi, Wenyeviti na Makatibu wa matawi, vijana na Wazee wa CCM katika ziara zake alizofanya hivi karibuni huko katika Wilaya ya Mfenesini Kichama kwenye Ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu za Mwl.Nyerere Tawi la Zanzibar Bububu.
Katika ziara hizo zlizokuwa na lengo la kuwashukru wafuasi wa Chama na wananchi kwa ujumla walioichagua CCM kwenye uchaguzi Mkuu wa Marudio uliofanyika Machi 20 mwaka huu pamoja na kuimarisha kuongeza kasi za kiutendaji ndani ya Chama, Dk.Shein aliwataka wananchi kupuuza kauli na misimamo ya wapinzani hasa Maalim Seif kwani hoja zao hazina nia ya kuwaunganisha wananchi bali ni za utengano.
Dk.Shein alisema, bango lililobebwa na Maalim Seif lililokuwa likimtangaza rais wa Zanzibar kuwa ni dikteta ni moja ya siasa zilizopitwa na wakati na kupingana na dhamira ya kuanzishwa kwa Mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, ulioasisiwa kwa nia ya kufanya siasa za uchumi na maendeleo kwa wananchi wote bila ya ubaguzi.
“Mimi sio dikteta kwani sijaingia madarakani kwa ubabe na mabavu kilichoniweka madarakani ni nguvu ya umma kupitia Uchaguzi wa Kidemokrasia na kupata ushindi wa zaidi ya asilimia 91," alisema Dk.Shein na kuongeza:
"Sasa huyo anayenitangaza eti mimi ni dikteta kweli maana ya neno hilo anayajua ama anasema kuwaridhisha wafuasi wake, akae akijua kwamba hawezi kunichafua kwa njia hiyo kwani kinga yangu ni Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 niliyoapa kuilinda na kuwatumikia wananchi kwa uadilifu.”
MWISHO
KISHA NYINYI MUNAYAITA MAPINDUZI MATUKUFU HIVI KWELI NYINYI MUNAJUWA UTUKUFU NI NINI AU DUNIA IMEWAVA KISAWA SAWA MPAKA MNAKUFURU MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA KATUPINDUWA TENA WAZANZIBARI NA KUWEKA VIONGOZI WAWATAKAO WAO WAKINA BT TUNAENDELEA TENA KUKA CHINI YA SERIKALI YA KIKOLONI YA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA MPAKA MIAKA MITANO IMALIZIKE KISHA TUTIWE TENA KATIKA SHENGESHA LA UCHAGUZI NA KUPIGA KURA KISHA WAZANZIBARI WAPIGE KURA NA KUCHAGUWA VIONGOZI WAWATAKAO MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA ATAKUJA NA STYLE MPYA YA KUZIPIGA KURA ZA WAZANZIBARI CHINI NA KUTUEKEA VIONGOZI WAWATAKAO KISHA TUTAKA TENA CHINI NA KUSUBIRI UCHAGUZI WA 2025 MAMBO YATAKUWA HIVYO HIVYO KISHA TUTAKA CHINA NA KUSUBIRI UCHAGU WA WA 2030 TUKIWA HAI KAMA HATUKO TENA WATAKAO BAKI WATAFANYIWA TENA HIVYO HIVYO NA MKOLONI MWEUSI TANGANYIKA KISHA WATAKA CHINI WASUBIRI......>>> MPAKA KIYAMA KISIMAME BASI NI BORA TU TUKUBALI KUWA NDIO TUMEKUBALI KUWA CHINI YA MKONI MWEUSI TANGANYIKA KULIKO UPUMBAVU HUU WA UCHAGUZI AMBAO KILA MOJA WETU HAPA ZANZIBAR KAMA UCHAGUZI WA MARA HII HAUJAWASOMESHA WALA HATUTA SOMA TENA MILELE.

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment