Thursday, July 14, 2016

AMIRI JESHI MKUU POMBE MAGUFULI ANAHUSIKA KWA ASILIMIA MIA MOJA NA MATATIZO YA UNYANYASAJI, MATESO NA KUWAWEKA MAHABUSU RAI WASIO NA HATIA YOYOTE KISIWANI UNGUJA NA PEMBA NA NCHINI KWAKE TANGANYIKA.



Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akiwa pamoja na Rais wa nchi ya Tanganyika Mkoloni Mweusi, Pombe Magufuli ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa nchini ya Tanganyika Wakoloni Weusi ((Tanzania.)) Zanzibar Pombe Magufuli (Amiri Jeshi Mkuu), anahusika kwa asilimia mia moja na matatizo ya unyanyasaji, mateso na kuwaweka mahabusi wananchi wa Pemba bila makosa. Ikumbukwe miaka 1990s: Wakati wa Utawala wa Komandoo Dk Salmini Amour (awamu ya tano) Polisi, Usalama wa Taifa na CCM kwa pamoja waliratibu uhalifu Kisiwani Pemba kwa kuvitia visima vya maji KINYESI. Kuzipaka kinyesi kuta na sakafu za maskuli pamoja na uharibifu mwingine huku, wakida vitendo hivyo vinafanywa na wafuasi wa CUF na Wapemba. Mwisho wa siku wananchi walipotaka kujuwa wahusika wa uhalifu huo walifanikiwa kuwakamata. Wananchi wa Zanzibar, hususan Pemba, wanasababu za kutosha kuamini kuwa hali inayoendelea Pemba, ni muendelezo wa uhalifu wa Polisi, Usalama wa Taifa na CCM. Tunaamini kwamba ya arobaini yao itafika na watakamatwa. Hakuna Mzanzibari mwenye akili yake timamu anaweza kuliamini Jeshi la Polisi. Hapa inamaanishwa kwamba uonevu wa raia Unguja na Pemba, haukuanza jana. Uonevu ni sera ya CCM na serikali zake.
Kinachofanyika sasa ni mbinu ili ipatikane sababu ya kuweza kumkamata na kumuweka ndani Maalim Seif, kosa lake ni kupendwa na Wazanzibari. Hajatokea Zanzibar, mtawala hata mmoja anayeweza kufananishwa na Maalim Seif. Maalim Seif ni mtu muungwana, mwadilifu na mwenye kuumizwa na nchi yake (Kipenzi cha nyoyo za Wazanzibari) na ndiyo maana CCM wanamtafutia vijisababu uchwara wamkamate. Hayo ni mambo yanayojuilikana wala si mageni tena kwa Wazanzibari. Soma habari iliyopo chini ili uweze kufahamu maelezo ya hapa juu kinachoendelea sasa Pemba. Pia, chuki ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Hamdani Omar Makame jinsi anavyomuandalia Maalim Seif ubaya kwa matakwa ya mabwana zake. Hamdani Omar Makame, kadiri anayojitahidi kuandaa ubaya dhidi ya Maalim Seif, atambue kuwa Maalim Seif na Wazanzibari wote wanaoitakia mema nchi yao, wamesimama na Kamba Mwenyezi Mungu Sub’hanahu Wataala. Wazanzibari hawamuogopi Magufuli, Kikwete, Shein na nduli Seif Ali Iddi (laana za Mwenyezi Mungu ziwashukie wote -amin.“Ukiona kiza cha usiku kimekuwa kinene…ujuwe alfajiri inakaribia.” Hiyo ni kauli ya Maalim Seif Sharif Hamad, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), aliyoitoa wakati akizungumza kwenye Baraza la Eid el Fitr, lililoandaliwa na CUF. Maalim Seif alitumia msemo huo akiimanisha kuwa, harakati za kudai haki yao ambayo anaamini kuwa iliporwa Oktoba 25, katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana imeanza kuonekana na muda sio mrefu itapatikana. Aliwatoa hofu na wasiwasi wafuasi na wanachama wa CUF na Wazanzibari, huku akisisitiza kuwa haki yao iliyoporwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), kwa kushirikiana na watawala muda si mrefu itapatikana. Maalim Seif anaamini kuwa yeye ndiye aliyeshinda wa uchaguzi wa Oktoba 25. “Haki ya mtu haipotei wala haizami, na haki yetu tuliyoporwa Oktoba 25 mwaka jana haipotei, ipo inaelea wala haijazama hivyo muda sio mrefu itapatikana na watawala wataondoka madarakani” alisema Maalim Seif.Alisema kuwa kitendo cha ZEC kufuta uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, kimesababisha mgawanyiko mkubwa Zanzibar, hali iliyosababisha vyombo vya dola, likiwamo jeshi la polisi kuwaadhibu wafuasi wa CUF na viongozi wao bila ya hatia yoyote. Alisema, wafuasi wa CUF na viongozi wao hasa kisiwani Pemba, wamekuwa wakikamatwa ovyo na kuadhibiwa na jeshi la polisi, kwa madai ya kufanya vitendo mbalimbali vya hujuma, kama vile ukataji wa mikarafuu na migomba. Maalim Seif akaongeza kuwa, hujuma zinazofanywa Pemba ni njama za makusudi zilizoandaliwa na wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kwa lengo la kuwabambikia kesi viongozi na wafuasi wa CUF. Na akaishtumu CCM kuwa ndiyo inayofanya hujuma hizo kwa makusudi kisiwani Pemba, ili aonekane yeye kuwa ndiye anayewatuma wafuasi wake kufanya hujuma hizo.Na kwamba hujuma hizo ndizo zinazosababisha kukamatwa wafuasi na viongozi wa CUF, kuwekwa ndani na kufanyiwa dhulma mbalimbali za udhalilishaji.“Vitendo vya hujuma wamekuwa wakifanya wenyewe CCM na kuwabambikia kesi wafuasi wa CUF, na wanapokamatwa na polisi huwatesa na kuwalazimisha wakubali,” alisema Maalim Seif na kuongeza: “Wanawalazimisha waseme kuwa wanatekeleza maagizo ya Katibu Mkuu yaani mimi…hivi ni lini mimi nilisema wana CUF wakate mikarafuu au migomba au hujuma zingine?…huo ni uzandiki tu.” Katibu Mkuu huyo ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar (mstaafu), akaongeza kuwa, kimsingi muelekeo ya yote hayo ni wa kumkamata yeye, kumshtaki na kumuweka ndani. “Mwanzo walitaka kunishtaki mimi kwa kosa la uhaini, lakini kwa mujibu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, huwezi ukafanya uhaini Zanzibar, na kwa hiyo sasa wanajielekeza kutaka kunifungulia makosa ya kuhujumu uchumi na makosa ya mtandao,” alisema na kuongeza:“Niwaambie kwamba hawana haja ya kuwatesa watu mimi nipo waje wanikamate tu wafunguwe mashtaka yao,” alisema Maalim Seif. Maalim Seif alimshangaa sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli kwa kitendo cha kumsifu Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha kwa kazi nzuri aliyoifanya. Hiyo ilikuwa wakati Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ilipokabidhi ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, ambapo Rais Magufuli alimpongeza Jecha kwa kazi nzuri aliyoifanya Zanzibar. Lakini Maalim Seif anasema: 

SAFARI YA MAREKANI

“Kitendo alichokifanya Mwenyekiti huyo ni ukiukwaji wa katiba,” alisema na kuongeza: “Rais wa nchi anadiriki kumpa sifa aliyekiuka katiba ya nchi…ndio hali yetu ilivyo kwa sasa, kwani hata wale askari wanaotesa watu Pemba, wameletwa kwa makusudi kutoka Bara.” Maalim alilaani kwamba, kukamatwa kwa wafuasi wake kumewanyima fursa ya kuwa na familia zao wakati huo wa sikukuu ya Eid, na kuwa wamewekwa ndani kinyume na sheria na hata hawapelekwi mahakamani.Hata hivyo alisema, pamoja na dhuluma zote hizo, watahakikisha kwamba wanaitafuta haki yao iliyoporwa kwa njia ya amani kwa uchaguzi halali wa Oktoba 25, uliyofutwa.
Akizungumzia safari yake ya mwezi uliopita, nchini Marekani na Canada, Maalim Seif alisema kuwa pamoja na nchi hizo kuwa na balozi zake Tanzania, bado zipo mstari wa mbele kuona demokrasia inaheshimiwa. Alisema lengo la safari hiyo lilikuwa kwenda kukutana na watunga sera wa nchi hizo, na kwamba walipata mapokezi mazuri kutoka kwa viongozi wa nchi hizo. Aidha, walipokewa vizuri pia na taasisi zinazoshughulikia masuala ya haki za binadamu, usalama na demokrasia na kwamba safari yao hiyo ilikuwa ya mafanikio makubwa.
Hata hivyo, alisema kuwa juhudi za kudai haki yao zinaendelea na kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, muda si mrefu watafika walipokusudia na kwamba viongozi waliyopo madarakani, wanapaswa kujua kuwa siku zao zinahesabika.Pia, Maalim Seif aliendelea kusisitiza kuhusu msimamo wa chama hicho wa kutokuitambua serikali ya SMZ inayoongozwa na Dk. Ali Mohamed Shein: “Na wasidhani kwa kuwatesa na kuwahoji wafuasi wa CUF, tutarudi nyuma, bali tunazidi kukaza kamba katika kudai haki yetu, kwa njia za amani,” alisema Maalim Seif.SHARTI LA MUAFAKA
Maalim seif alisema, ili muafaka upatikane ni lazima Rais aliyepo madarakani, Dk. Shein aondoke, iundwe serikali ya mpito na hatimaye ufanyike uchaguzi mwingine, utakaosimamiwa na mataifa ya nje, si ZEC inayoongozwa na Jecha.JESHI LA POLISI NA KAMATAKAMATA PEMBA NA UNGUJA.

Jeshi la Polisi Zanzibar, limesema vitendo vya kihalifu Pemba, vimezuka kufuatia kauli ya uchochezi ya Maalim Seif, wakati alipofanya ziara ya kichama kisiwani humo.Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Hamdani Omar Makame amesema kuwa, kufuatia kauli ya Katibu Mkuu huyo ndipo vitendo vya hujuma na kuhasimiana vilipoanza kushamiri na kusababisha hofu kwa wananchi na jamii nzima kwa ujumla.

“Hali hiyo ndiyo iliyolifanya jeshi la polisi kuanzisha operesheni maalum ya kupambana na vitendo hivyo vya kihalifu, ikiwa ni pamoja na kuwakamata watuhumiwa waliohusika na vitendo hivyo, kuwahoji na hatimaye kuwafikisha mahakamani,” alisema Hamdani.

Alisema kuwa jambo la kushangaza ni kauli zinatolewa na baadhi ya viongozi hasa wa vyama vya upinzani kuwa watu wanaokamatwa kuhusiana na tuhuma hizo ni wafuasi wa CUF pekee, jambo ambalo si kweli.Hamdani alisema jeshi la polisi linafanya shughuli zake kitaalamu na kwa mujibu wa sheria na kamwe halijihusishi na masuala ya kisiasa kama ilivyoelezwa ndani ya katiba na sheria za nchi.“Jeshi la polisi linashughulika na wahalifu na wala halimuulizi mtuhumiwa ana itikadi gani, kabla na baada ya kumkamata, ”alisema Hamdani.Aliwaasa wanasiasa wasiliingize jeshi hilo katika malumbano yao ya kisiasa na badala yake watekeleze jukumu lao la kuwaelimisha na kuwasihi wanachama na wafuasi wao waepuke kujiingiza katika vitendo vya uhalifu.Alisema kuwa haingii akilini kiongozi anayeshawishi wafuasi wake kutenda maovu, kisha kiongozi huyohuyo anaanza kupiga kelele na kulaumu, pale wanapokumbwa na mkono wa vyombo vya dola.Alitoa onyo kwa wote wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu kwamba mapambano dhidi yao ni endelevu na ya kudumu na watambue kuwa wanapokamatwa watafikishwa mahakamani.“Na wakati nyie mkienda peke yenu, viongozi waliyowashawishi kufanya vitendo vya kihalifu watakuwa wakiendelea na shughuli zao kama kawaida bila ya kujali kitu chochote,” alisema Hamdani.

No comments:

Post a Comment