Tuesday, November 8, 2016

VIDEO-YULE SAMUEL SITTA AFARIKI DUNIA NA KUIWACHA NCHI YA ZANZIBAR HAPA HAPA KAMA ALIVYO IWACHA NYERERE NA WENGINE WANAO TAKA KUIMALIZA NA KUIDIDIMIZA NCHI YA ZANZIBAR.

HE: SITTA MEETS DIASPORA UK [PART 3]
HE: SITTA MEETS DIASPORA UK [PART 4]
Dar es Salaam. Spika wa Bunge Mstaafu, Samuel Sitta (74) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo wakati akipatiwa matibabu nchini Ujerumani.
Mtoto wa marehemu, Benjamin Sitta amesema baba yake amefariki saa 10:00 usiku wa kuamkia leo.
‘’Nikweli mzee amefariki nchini Ujerumani akiwa anapatiwa matibabu, alipelekwa Alhamisi iliyopita na alikuwa anasumbulia na saratani ya tezi dume ambayo ilisambaa na kuathiri miguu na mwili mzima.
Benjamin amesema kuwa taarifa za mipango ya kusafirisha mwili zitatolewa baadaye.
Sitta alikuwa Spika wa Bunge tangu mwaka 2005 hadi mwaka 2010 na pia mbunge wa Urambo Mashariki.
Pia, alikuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba na aliwahi kuwa waziri katika wizara mbalimbali kwa vipindi tofauti.

No comments:

Post a Comment