Sunday, December 11, 2016

BWANA SALIM SAID RASHID MWITO KWA WAZANZIBARI WOTE

IMG_4754
Nimepokea ujumbe ufuatayo kutoka kwa Bwana Salim Said Rashid, Katibu wa Kwanza wa Baraza la Mapiduzi, Januari 1964 Zanzibar:
MWITO KWA WAZANZIBARI
Kwa muda mrefu mpaka hivi sasa hali halisi ya Zanzibar kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni hairidhishi. Wazanzibari walilazimika kustahmili kutokana na matumizi ya jeshi na polisi kwa sababu za kisiasa wameogopa kuyatetea maslahi ya nchi yao tajiri yenye historia ya takriban miaka elfu mbili kama ilivoyo andikwa na mwana historia wa Kigreeki baada ya kufanya ziara ya Zanzibar wakati huwo. Hali hii ambayo ilianza tarehe 26 April 1964 ulivyo asisiwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na Mwalimu Nyerere na kuifanya Zanzibar isite kua taifa huru Mwanachama wa Umoja wa Mataifa. Ikawa kikatiba haina mamlaka ya mwisho ya kufanya maamuzi ya mambo yake ya ndani na nje kuliko ilivyokua wakati ikitawaliwa na mkoloni wa Kingereza. Baada ya shinikizo kutoka mashirika ya kimataifa na khusuusan mataifa ya magharibi na madai ya Wazanzibari ya mfumo wa vyama vingi hapa Zanzibar umeanzishwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Kwa bahati mbaya tangu kuanzishwa na mkoloni wa Kingereza utaratibu wa vyama vingi vya kisiasa 1957 Zanzibar imeingia katika migogoro ya kisiasa baina ya vyama viwili na kuyapa fursa mataifa ya kigeni kama vile Tanganyika kuwa na uwezo wa kuifutia madaraka na mamlaka Zanzibar kama ilivyo fanya Hati ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar ambao umeleta madhara makubwa kwa vile Zanzibar imesita kuwa na uwezo kamili wa kujitawala kama inavyo stahili. Wakati umefika wa kila Mzanzibari kutathmini Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutazama athari mbaya kwa Wazanzibari na taifa lao. Kwa vile Muungano haukupata ridhaa ya Wazanzibari ambao ili bidi washirikishwe katika suala muhimu kama hili la kupoteza mamlaka ya nchi yao Wazanzibari waiombe Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iitishe kwa mujib ya sheria ya Zanzibar kura ya maoni mapema iwezekanavyo bila ya kujali itikadi za vyama vya kisiasa endapo wanataka kuendelea na Muungano au wanapendelea Uhuru wa Zanzibar.
Salim Said Rashid, Katibu wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi, January 1964

No comments:

Post a Comment