Saturday, January 21, 2017

YAHYA JAMMEH AKUBALI KUACHIA MADARAKA NCHINI GAMBIA JE SHEIN KIGHAGHANIZI UTACHIA LINI MADARAKA AU MPAKA WAZANZIBARI WAJAE IKULU KUJA KUKUSADIA KUHAMA...??

Afbeeldingsresultaat voor Adama Barrow akiwa na wake zake
Afbeeldingsresultaat voor dr shein akataliwa mkono wake na maalim seif
Yahya Jammeh ambaye amekua madarakani na kuingoza Gambia kama Rais kwa miaka 22 hatimae amekubali kuachia madaraka hayo na sasa Adama Barrow aliyetangazwa mshindi kwenye uchaguzi mkuu ndio anatarajiwa kuchukua nafasi.

Kupitia Television ya taifa, Yahya ametangaza kuachia madaraka ambapo AlJAZEERA wameripoti kwamba taarifa kutoka IKULU zilisema baada ya kuachia madaraka alitarajiwa kuondoka kwenye nchi hiyo ndani ya siku 3 ila media nyingine zinasema amepewa saa tu za kuondoka.
Afbeeldingsresultaat voor Yahya Jammeh
TV ya habari Nigeria imesema ECOWAS walimpa hadi saa sita mchana kuondoka lakini mwenyewe akaomba muda huo usogezwe hadi saa kumi jioni na imeripotiwa atakwenda kuishi Guinea.

Barrow aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter na kusema ‘Yahya Jammeh amekubali kuachia madaraka na anatarajiwa kuondoka kwenye nchi ya Gambia leo’.

No comments:

Post a Comment